Saturday , 15 June 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Zitto amjibu Lissu ‘inawezekana’
Habari za Siasa

Zitto amjibu Lissu ‘inawezekana’

Spread the love

OMBI la Tundu Lissu, mgombea urais wa Tanzania kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), aungwe mkono na Chama cha ACT-Wazalendo kwa upande wa Tanzania Bara, linafanyiwa kazi. Anaandika Mwandishi Wetu, Zanzibar…(endelea).

“…tutaafikiana kuhusu mgombea mmoja wa urais kupigiwa kura na Watanzania wote,” amesema Zitto Kabwe, Kiongozi wa ACT-Wazalendo wakati akizungumza na gazeti moja la kila siku tarehe 13 Septemba 2020.

Lissu alipokutana na baadhi ya wahariri na waandishi waandamizi nyumbani kwake Tegeta, jijini Dar es Salaam hivi karibuni, alieleza namna chama chake kilivyoafikiana kumuunga mkono Maalim Seif Sharif Hamad, mgombea urais visiwani Zanzibar kupitia ACT-Wazalendo.

“Kule Zanzibar kuna pande mbili, ukiunga mkono Muungano huu wa sasa wewe ni CCM, ukipinga wewe ni ACT-Wazalendo, na sisi tunaupinga huu wa sasa maana yake tunamuunga mkono Maalim Seif.”

“Tunaunga mkono chama chenye nguvu ya kuiondoa CCM madarakani, sasa na sisi tunawaambia wenzetu waunge mkono chama chenye nguvu ya kuishinda CCM Bara. Sisi Zanzibar tunaweza kuokoteza kura lakini hatuwezi kushinda,” alisema Lissu bila kutaja chama hicho.

Tundu Lissu, Mgombea Urais Tanzania kwa tiketi ya Chadema

Zitto amesema, mazungumzo na Chadema yamekwenda mbali zaidi na hata kuachiana majimbo ili upinzani uweze kupata ushindi.

“Mazungumzo yanaendelea ili kuungana mkono kwa wagombea ambao wanakubalika hata kwenye majimbo ili tuweze kushinda,” amesema.

Bernard Membe, mwanachama mpya wa ACT-Wazalendo na mgombea urais kupitia chama hicho wakati akitambulishwa kwa wanachama, kwenye ukumbi wa Mlimani City, jijini Dar es Salaam alisema, endapo atatokea mgombea mwingine anayekubalika, yupo tayari kumwachia apambane na CCM.

Membe ambaye ni mshauri mkuu wa chama hicho, ndiye aliyeteuliwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kuwa mgombea urais katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Jumatano tarehe 28 Oktoba 2020.

Tayari amekwisha zindua kampeni za urais Mkoa wa Lindi na kufanya mikutano kadhaa mkoani humo na Mtwara.

Hata hivyo, ni zaidi ya wiki moja sasa kampeni zake zimesimama, Arodia Petet, Ofisa Habari wa ACT-Wazalendo alipoulizwa kuhusu kusimama kwa kampeni alisema “kuna mambo yamejitokeza na kwa sasa tunarekebisha ratiba na kisha tuipeleke tume ili tuendeleee na kampeni.”

2 Comments

  • Upinzani TZ haioneshi kama kuna nia ya dhati kuiondoa ccm madarakani! Kwa nn hamuungani kikamilifu kuanzia ubunge hadi urais?
    Kwa hali hii mi naona tutasubiri saaana!!!

  • Wapiga deal hao hakuna lolote, fika wanajua hawezi kuiondoa CCM madarakani hata wafanye nn kilichobaki ni vp watapata chance ya kukusanya ruzuku through wabunge. Siasa za upinzani Tanzania ni matumbo tuu wangetakiwa tangia waliposhindwa 2015 wakae chini wajipange na kuunda chama dhabiti kuikabili CCM. Mwenye akili timamu atakuwa wazimu kuwapigia kura watu ambao hata hawajielewi, wachache wasiojua nini kinaendelea Tanzania ndio watakaowapigia kura.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari za Siasa

Tanesco yawasha mtambo namba 8 Bwawa Julius Nyerere

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

Habari MchanganyikoHabari za SiasaTangulizi

Samia: Wakuu wa mikoa, wilaya wanaendeleza ubabe

Spread the loveRAIS Samia Suluhu Hassan amesema bado wakuu wa wilaya na...

Habari za SiasaKimataifaTangulizi

Ramaphosa achaguliwa tena kuwa rais Afrika Kusini

Spread the loveRais wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa amechaguliwa na wabunge wa...

Habari za SiasaKimataifaTangulizi

DA, ANC waridhia kuunda serikali ya mseto Afrika Kusini

Spread the loveChama tawala nchini Afrika Kusini cha African National Congress, ANC,...

error: Content is protected !!