Thursday , 7 December 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Dk. Bashiru: Magufuli akimaliza miaka 10 anaondoka
Habari za Siasa

Dk. Bashiru: Magufuli akimaliza miaka 10 anaondoka

Aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) nchini Tanzania, Dk. Bashiru Ally
Spread the love

JOHN Pombe Magufuli, Rais wa Tanzania hataongeza muda wa kukaa madarakani pindi vipindi vyake viwili vya Serikali ya awamu wa Ttno vitafika ukomo. Anaripoti Mwandishi Wetu, Chato … (endelea).

Hayo yamesemwa leo tarehe 14 Septemba 2020 na Dk. Bashiru Ally, Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), katika mkutano wa kampeni za Urais uliofanyika Uwanja wa Mazaina wilayani Chato Mkoa wa Geita.

Dk. Bashiru akihutubia umati wa wananchi kwenye mkutano huo amesema,
madai ya kwamba chama hicho kinataka kupata viti vingi vya ubunge ili Katiba ibadilishwe kwa dhumuni la kumuongezea muda Rais Magufuli ni uongo, kwani akimaliza muda wake hataongoza hata sekunde.

“Mwisho kabisa nitumie jukwaa hili ambalo wewe unazaliwa kukanusha kidogo uvumi kwamba eti CCM inataka kushinda viti vingi vya ubunge ili tubadilishe katiba uongezewe muda, nalisema hili mara ya mwisho maana yake wewe hapa ndipo kuna mizimu yako na baraka zako,” amesema Dk. Bashiru.
Rais Magufuli ni mzaliwa wa Chato mkoani Geita.

Dk. Bashiru amewaomba Watanzania wamchague Rais Magufuli ambaye pia ni Mgombea Urais wa Tanzania kupitia CCM, ili akamilishe vipindi vyake viwili vya uongozi.

Dk. Bashiru amesisitiza kuwa “umekanusha mara nyingi lakini watu waliochoka na kufilisika kisiasa wanaendelea kutuchokonoa, ameshasema na naomba kusisitiza anaomba miaka mitano iikamilike 10 na akimaliza hataongeza hata sekunde, mbona hiyo sentensi ni nyepesi.”

Aidha, Dk. Bashiru amemuomba Rais Magufuli kutokuwa na huruma katika uongozi wake.

“Nikupongeze kwa kazi unayofanya na nikukabidhi raundi ya pili, wewe ndio unayetuongoza usiwe na huruma na mtu yeyote wamejileta wenyewe, wakimbilie kulia wewe nenda kushoto. Waende nje piga hapa hapa mpaka wapate adabu,” amesema Dk. Bashiru.

Rais Magufuli anayemaliza muda wake katika kipindi chake cha kwanza cha uongozi, aliingia madarakani tarehe 5 Novemba 2015, baada ya kushinda katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka huo, ambapo alipokea kijiti hicho kutoka kwa Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa awamu ya nne.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Bashungwa: Katesh kutafanyiwa usafi wa hali ya juu

Spread the loveWAZIRI wa Ujenzi, Innocent Bashungwa amesema kazi ya kuondoa tope...

AfyaHabari za Siasa

RAS Songwe: Tumepigwa… mkurugenzi nakupa siku 21

Spread the loveKATIBU tawala mkoani Songwe, Happines Seneda ametoa siku 21 kwa...

Habari za Siasa

Dk. Biteko: Viongozi tuache alama nzuri katika utendaji wetu

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

Habari za SiasaTangulizi

Chanzo maporomoko yaliyoua 65 Hanang, chatajwa

Spread the loveSERIKALI imesema kumeguka kwa sehemu ya Mlima Hanang ambao ilikuwa...

error: Content is protected !!