Friday , 17 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Zitto akambushia maumivu ya uchaguzi mkuu 2020
Habari za SiasaTangulizi

Zitto akambushia maumivu ya uchaguzi mkuu 2020

Spread the love

 

KIONGOZI wa chama cha siasa cha upinzani cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe amekumbushia machungu ya uchaguzi mkuu uliopita wa Oktoba 2020 akisema, chama hicho kiliumizwa vilivyo. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Zitto amesema hayo leo Jumapili, tarehe 31 Oktoba 2021, katika kikao cha Halmashauri Kuu ya ACT-Wazalendo, unaofanyika Holet ya Landmark jijini Dar es Salaam.

“Katika mwaka huu mmoja uliopita, Watanzania tumepita na tunaendelea kupita katika misukosuko mikubwa iliyosababishwa na utawala wa kikandamizaji wa Chama Cha Mapinduzi (CCM),” amesema Zitto

“Makundi mbalimbali ya jamii yameumizwa na maamuzi na matendo ya Watawala – kuanzia wakosoaji wa Serikali, vyama vya Siasa, Asasi za Kiraia mpaka wananchi wa kawaida kabisa kama Wakulima na Wafugaji,” amesema.

Zitto amesema, ulikuwa uchaguzi mbaya zaidi tangu kurudishwa kwa siasa za vyama vingi mwaka 1992.

“Ni uchaguzi ambao vyama vya upinzani vilipambana na vyombo vya Dola kwa niaba ya CCM. Ulikuwa ni uchaguzi wa kuirudisha nchi yetu kwenye Mfumo wa Chama kimoja, kabla ya mwaka 1992,” amesema

Amesema “chama chetu, wanachama na wafuasi wetu, ndio wahanga wakubwa zaidi wa madhila ya uchaguzi huu kuliko chama kingine chochote cha siasa nchini.”

“Wanachama wetu Zaidi ya 270 wakapigwa na kuachwa na majeraha mbalimbali, Mjumbe mwenzetu wa Halmashauri Kuu, ndugu Ismail Jussa ni kielelezo cha wanachama wetu hao, huku viongozi wetu zaidi ya 42 wakitekwa na kupelekwa kusikojulikana, Naibu Katibu Mkuu wetu Zanzibar, Nassor Mazrui ni kielelezo cha kundi hili. Uchaguzi ule ni kumbukumbu zenye kuacha uchungu mkubwa mno kwetu,” amesema Zitto.

Amesema, madhila hayo hayakuishia Zanzibar tu, hata bara yaliendelea, “nitatoa mfano mmoja muhimu sana, kule Liwale wanachama wetu mbalimbali walifunguliwa kesi za kubambikiwa (utakatishaji fedha na unyangányi wa kutumia silaha) baada ya kuonekana wanapinga matokeo ya uchaguzi ule ulioharibiwa, mwanachama wetu Mawazo Khalid Magumba ndiye aliyekuwa Kiongozi wa hawa waliobambikiwa mashtaka.”

“Lakini siku aliyokwenda kukamatwa nyumbani kwake, Polisi walimuua kwa kumpiga risasi mkewe, Aziza Chande Kibou, na mtoto wao mchanga akabaki bila mama huku baba akiwa jela. Tarehe 13 Oktoba mwaka huu Mahakama imewaachia huru Mawazo na wenzake, kutoka kwenye mashtaka yale ya kubambikiwa, amerudi nyumbani mkewe hayupo, na ameachiwa mtoto mchanga wa kulea. Ni mambo ya kuumiza sana,” amesema

Zitto amesema “matokeo ya uchaguzi huu yalikuwa ni ACT Wazalendo ‘kupewa’wabunge wanne, pamoja na wawakilishi wanne. Tunajua, hiki sicho tulichostahiki.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Udhibiti wa serikali wakera asasi za kiraia

Spread the loveBaadhi ya wadau wa demokrasia na viongozi wa asasi za...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Nape aomba bajeti ‘kiduchu’ kwa mwaka 2024/25

Spread the loveWaziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Seneta: Wanasiasa hawasaidii mchakato wa Katiba mpya

Spread the loveSeneta wa jimbo la Busia, nchini Kenya, Okiya Okoiti Andrew...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

ACT-Wazalendo yasusia uchaguzi wa ubunge Zanzibar

Spread the loveCHAMA cha ACT-Wazalendo, kimegoma kushiriki uchaguzi mdogo wa Ubunge Jimbo...

error: Content is protected !!