Friday , 1 March 2024
Home Kitengo Michezo Yanga yaachana na Yondani na Juma Abdul
Michezo

Yanga yaachana na Yondani na Juma Abdul

Spread the love

KLABU ya Yanga leo imetangaza rasmi kuachana na wachezaji wake wakongwe, Kelvin Yondani na Juma Abdul baada ya kutofikia makubaliano baada ya mikataba yao kumalizika baada ya msimu kumalizika. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea).

Hivi karibuni klabu hiyo ilitangaza kuwa katika mazungumzo na wachezaji hao wawili baada ya kutoa taarifa ya wachezaji wao walioachana nao kwa baadhi yao kuvunjiwa mikataba na wengine mikataba kumalizika.

Taarifa kutoka ndani ya klabu hiyo, imeeleza kuwa, uongozi umeshindwa kufikia makubaliano na wachezaji hao na kuwaruhusu kuondoka ndani ya kikosi hicho na kutafuta timu nyingine.

Yondani amedumu ndani ya kikosi cha Yanga kwa miaka nane, baada ya kujiunga na klabu hiyo mwaka 2012 akitokea Simba ambapo alicheza kwa miaka sita na kufanikiwa kushinda mataji mbalimbali.

Naye Juma Abdul ambaye ni beki wa upande wa kulia amedumu ndani ya kikosi hicho kwa miaka nane baada ya kujiunga na timu hiyo mwaka 2012 akitokea Mtibwa Sugar.

Klabu hiyo ambayo mpaka sasa itakuwa imeacha jumla ya wachezaji 19 nakusalia na wachezaji 17 pekee ambao wataingia kambini kuanzia tarehe 10 Agosti, 2020 ili kujiandaa na msimu ujao wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Mpaka sasa Yanga imesajili wachezaji wandani watano katika kuboresha kikosi chao kuelekea msimu ujao wa Ligi ambao ni Bakari Mwamnyeto, Wazir Junior, Zawadi Mauya, Yassin na Abdalah Shaibu (Ninja)

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

Wizara yaahidi kuboresha, kuimarisha michezo

Spread the loveIkiwa ni saa kadhaa baada ya kumalizika kwa mashindano ya...

Habari MchanganyikoMichezo

Nje jogging yanyakua medali 20 Kili Marathon

Spread the loveTimu ya riadha ya Wizara ya Mambo ya Nje na...

Michezo

Siku ya kukusanya maokoto ni leo, usipange kukosa

Spread the love  HATIMAYE Jumamosi imefika ndugu mteja wa Meridianbet na mechi...

Michezo

Kuwa milionea na Meridianbet ni rahisi sana

Spread the love  JE, unajua kuwa leo hii ni siku nzuri kwako...

error: Content is protected !!