April 14, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Yanga, Simba wamlilia Mzee Akilimali

Marehemu Mzee Ibrahim Akilimali

Spread the love

KLABU ya Yanga imemlilia aliyekuwa Katibu wa Baraza la Wazee wa klabu ya Yanga, Mzee Ibrahim Akilimali, aliyefariki dunia alfajiri ya leo tarehe 14 Desemba 2019, Bagamoyo mkoani Pwani. Anaripoti Kelvin Mwaipungu … (endelea).

Kwa mujibu wa taarifa ya klabu hiyo iliyotolea asubuhi ya leo, Mzee Akilimali atazikwa kesho tarehe 15 Desemba, 2019 majira ya saa 10 jioni, maeneo ya Tandale kwa Mtogole.

“Klabu ya Yanga inasikitika kutangaza kifo cha Mwanachama wetu Maarufu na Mzee wetu, Ibrahim Akilimali kilichotokea alfajiri ya leo Bagamoyo Mkoani Pwani. Maziko yanatarajiwa kufanyika kesho saa 10 jioni Tandale kwa Mtogole. Innah lillah wainnah ilayh rajiuun. Haikuwa Dunia ila ni mapito,” inaeleza taarifa ya Klabu yaYanga

Haji Manara, Afisa Habari wa Klabu ya Simba ametoa pole kwa familia ya Mzee Akilimali kwa msiba huo mzito.

Pia, Manara amesema Simba itashiriki kikamilifu kwenye msiba huo.

“Tumeondokewa, Mwamba katika Miamba ya kabumbu Nchini umeanguka, Mzee wetu, Baba na Babu yetu, Katibu wa Baraza la Wazee, Yanga Ibrahim Akilimali katangulia mbele ya haki, poleni Familia, poleni Wanayanga,huu ni msiba wetu sote na tutashiriki kikamilifu kwenye majonzi haya,” amesema Manara.

error: Content is protected !!