July 7, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Yanga mmmh!! kocha, naodha waliamsha

Lamine Moro, Nahodha wa Yanga

Spread the love

Ni kama huko ndani ya klabu ya Yanga, kumekuwa na hali yasintofahamu mara baada ya kuwepo kwa taarifa za kuomba kuondoka nahodha wa kikosi hiko, Lamine Moro raia wa Ghana, huku wakati huo huo kocha wa timu ya wanawake Edna Lema kuvunja mkataba na klabu hiyo na kutimkia Fountain Gate ya jijini Mwanza. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea)

Lamine ambaye hivi karibuni ameonekana kuwa katika matitizo na benchi la ufundi la klabui hiyo, mara baada ya kuripotiwa kuwa na matendo ya utovu wa nidhamu.

Taarifa kutoka ndani ya klabu hiyo zimeeleza kuwa, nahodha huyo anataka kuvunja mkataba na Yanga, ambao umebakia kipindi cha mwaka mmoja kumalizika, ili kutafuta marisho sehemu nyingine kama ilivyokuwa kwa muangola Carlos Carmo ‘Carlinhos’.

“Lamine ameomba kuvunja mkataba, mara baada ya kuingia kwenye matatizo na kocha wa sasa Nassreddine Nabi, na kutopata nafasi kwenye kikosi cha kwanza kwa sasa”. Kilisema chanzo hiko.

Edna Lema, aliyekuwa kocha wa Yanga princes

Toka alipowasili kocha Nabi Aprili mwaka huu, hakuonekana kuvutiwa na tabia ya mchezaji huyo, kiasi cha kumlipoti kwa viongozi, mara baada ya kumrudisha Dar es Salaam, wakati timu hiyo ilipokuwa mkoani Lindi kwenye mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, dhidi ya Namungo FC, ambao ulimalizika kwa sare ya bila kufungana.

Kabla ya Lamine kuomba kuondoka tayari kocha huyo alishakili adharani kuwa amewaambia viongozi watafute beki mmoja wa kati katika dirisha kubwa la usajili litakalofunguliwa hivi karibuni.

Nabi alisema kuwa ameshawapa kazi mabosi wa Yanga kuwa, waandae listi ya usajili wa ajili ya msimu ujao na yeye atatoa mapendekezo ya idara gani ndani ya uwanja anayotaka ifanyiwe kazi, huku akikili kuihitaji beki mmoja wa kati kwenye kikosi chake.

“Niliwaambia viongozi waandae timu ya usajili, iliwatafute wachezaji, ila ni kweli nataka waongeze beki mmoja wa kati.” Alisema Nabi

Wakati sintofahamu ya Lamine Moro inaendelea hivi karibuni uongozi wa Yanga, ulikubari ombi la kujiudhuru kwa kocha wa ‘Yanga Princes’ Edna Lema mara baada ya kuhudumia timu hiyo kwa muda mrefu.

Ombi la kujiudhuru kwa kocha huyo ambaye pia ni moja ya makocha wa timu ya Taifa ya wanawake Twiga Stars, akihudumu kama kocha msaidizi.

Taarifa za kuaminika ambazo Raia Mwema imezipata ni kwa mba kocha huyo muda wowote kuanzia sasa, atatangazwa kama kocha mpya wa timu ya wanawake ya Fountan Gate, mara baada ya kuwekewa dau nono.

error: Content is protected !!