
RAIS wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, awaapisha Balozi Batlida Buriani kuwa Mku wa Mkoa wa Tabora (RC) na Zuwena Omari Jiri kuwa Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga (RAS). Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).
Shughuli hiyo imefanyika leo Jumatatu, tarehe 21 Juni 2021, Ikulu ya Chamwino, jijini Dodoma.
Kabla ya uteuzi wa Balozi Buriani, alikuwa Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga.
Ni baada ya mabadiliko madogo ya wakuu wa mikoa aliyoyafanya hivi karibuni.
Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa amewapongeza kwa kuteuliwa na kuwataka kwenda kusimamia “uchapakazi wenu. Kasimamieni watumishi huko ili kutoa huduma mbalimbali kwa Watanzania.”
“Watanzania wakiri kwamba Serikali yao inawatumikia. Tuna kipindi cha miaka mitano, wananchi wanatarajia kuona matokeo,” amesema Majaliwa.
Majaliwa amewataka watendaji wote wa Serikali kuhakikishia wanatekeleza majukumu yao kwa kufuata misingi ya utawala bora.
Katika shughuli hiyo, Rais Samia hakuzungumza zaidi ya kusema “mulioapishwa hongereni, kazi iendelee.”
More Stories
CCM yataka viingilio Sabasaba vipunguzwe
Maandalizi Sensa yafikia asilimia 87 zikiwa zimebaki siku 48
Mahakama yasema uamuzi kesi ya kina Mdee haujakamilika