Friday , 3 February 2023
Home Kitengo Michezo Yanga kutambulisha Benchi jipya la ufundi
Michezo

Yanga kutambulisha Benchi jipya la ufundi

Spread the love

 

KLABU ya Soka ya Yanga itaweka wazi benchi lake la ufundi kwenye kilele cha siku ya Mwananchi, mara baada ya kuwepo kwa taarifa za kuvunja mkataba kwa kocha wao msaidizi Sighr Hamad na mtaalamu wa mazoezi ya viungo Jawad Sabri. Anaripoti Wiston Josia na Ndelem Damas/TUDARCo…(endelea)

Timu hiyo kwa sasa imeweka kambi Rabat, nchini Morocco kwa ajili ya kufanya maandalizi ya msimu (Pre-Season), chini ya kocha wao Mkuu, Mohammed Nasreddin Nabi.

Yanga ambao watarejea nchini Agosti 27, kujiandaa na Tamasha lao kubwa la siku ya Mwananchi ambalo litafanyika Agosti 28, Mwaka huu, kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.

Hassan Bumbuli, Afisa Habari wa Yanga

Akizungumza na juu ya watu hao wa benchi la ufundi kuvunja mkataba, Afisa Habari na Mawasiliano wa klabu ya Yanga, Hassan Bumbuli alisema kuwa kuna baadhi yao wameshamaliza mikataba, hivyo wanaangalia

uwezekano wa kuwaongeza au kuachana nao, na siku ya kilele cha Tamasha hilo ndipo watakapojulikana rasmi.

“Mimi pia ni sehemu ya utambulisho siku hiyo, na utambulisho utakuwa mpaka kwenye benchi la ufundim kwa hiyo waandishi muwe wavumilivu”

“Kuna watu wamemaliza mkataba, kwa hiyo wanaweza kuwepo au wasiwepo, nap engine wanaweza kupewa mkataba mpya kama tukikubaliana kama tukikubaliana, tusipokubaliana hawata kuwepo” alisema Bumbuli

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

GGML: Uwanja mpya wa Geita Gold FC kukamilika Mei, 2023

Spread the loveUWANJA wa Magogo unaojengwa na Halmashauri ya Mji wa Geita...

Michezo

Wanafunzi chuo Mwalimu Nyerere wapongezwa kwa ushindi

Spread the love  UONGOZI wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere (MNMA)...

Michezo

Arsenal waipopoa Manchester United

Spread the loveKLABU ya Arsenal inayoshiriki Ligi Kuu England imewatandika Mashetani Wekundu...

Michezo

Mchezaji Singida apoteza maisha mazoezini

Spread the love  MCHEZAJI na kapteni wa timu ya vijana ya Singida...

error: Content is protected !!