Friday , 26 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Yametimia: Membe kuelekea ACT- Wazalendo
Habari za SiasaTangulizi

Yametimia: Membe kuelekea ACT- Wazalendo

Spread the love

SASA ni dhahiri kuwa Bernard Kamilius Membe, waziri wa zamani wa mambo ya nje na uhusiano wa kimataifa nchini Tanzania, yuko mbioni kujiunga na ACT – Wazalendo. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Kwa mujibu wa taarifa zilizothibitishwa na baadhi ya viongozi wandamizi wa ACT- Wazalendo zinasema, majadiliano kati ya mwanasiasa huyo na viongozi hao juu ya kujiunga kwake na chama hicho, tayari yamekamilika.

“Huyu bwana yuko njiani kujiunga na chama chake,” ameeleza mmoja wa viongozi wa ngazi ya juu wa chama hicho na kuongeza, “kila kitu kimekamilika na muda wowote kutoka sasa, atatangaza adhima hiyo.”

Picha kwenye mitandao ya kijamii zinawaonyesha viongozi wandamizi wa ACT- Wazalendo, wakiongozwa na Maalim Seif Shariff Hamad, wakiwa na majadiliano na mwanasiasa huyo, yenye lengo la kuweka mambo sawa.

MwanaHALISI Online halijaweza kumpata Membe wala viongozi wengine wandamizi wa ACT- Wazalendo, kueleza kwa undani ni lini kiongozi huyo atajiunga na chama chao.

Kupatikana kwa taarifa kuwa Membe yuko mbioni kujiunga na chama hicho cha upinzani nchini, kumekuja siku moja baada ya kilichokuwa chama chake – Chama Cha Mapinduzi – kutangaza kubariki maamuzi ya kumfuta uwanachama.

Membe alikuwa kwenye msuguano na CCM, tangu alipoonesha nia ya kutaka kumpinga rais wa sasa, Dk. John Pombe Magufuli, kupitia chama hicho.

Aidha, katika siku za hivi karibu, Membe amekuwa akitoa kauli zenye kukosoa mchakato wa utafutaji mgombea urais wa Tanzania ndani ya chama hicho tawala, kwa madai kuwa umegubikwa na vitisho.

Katika mahojiano yake na Idhaa ya Kiswahili ya Ujerumani (D.W), Membe alieleza kuwa takribani wanachama sita wa CCM walitaka kuchukua fomu ya kugombea nafasi hiyo ya juu nchini Tanzania, lakini waliogopa kufanya hivyo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Prof. Muhongo akomalia matumizi nishati jadidifu kuondoa uhaba wa umeme

Spread the love  MBUNGE wa Musoma Vijijini (CCM), Profesa Sospeter Muhongo, ameendelea...

Habari za Siasa

Kilosa yawa mfano wa kuigwa miradi ya Mwenge nchini

Spread the love  KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa Godfrey Mzava amezitaka...

Habari za SiasaTangulizi

Biteko ataja vipaumbele 7 bajeti nishati 2024/25

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mwekezaji amwaga bil. 39 kujenga viwanda 3 vya uchenjuaji

Spread the loveKampuni ya Mineral Access System Limited (MAST) inayoiwakilishwa kampuni ya...

error: Content is protected !!