Tuesday , 21 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Watumishi watakiwa kuwapa wananchi elimu ya madhara ya El-Nino
Habari Mchanganyiko

Watumishi watakiwa kuwapa wananchi elimu ya madhara ya El-Nino

Spread the love

 

WATUMISHI wa Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa, jijino Dodoma, wametakiwa kutoa elimu na maelekezo kwa wananchi juu ya namna ya kuchukua tahadhari na kujilinda dhidi ya athari za mvua kubwa ya El-Nino. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Wito huo ulitolewa jana tarehe 26 Oktoba 2023 na Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma, Ally Gugu, katika ziara yake ya kikazi, baada ya Mamlaka ya Utabiri wa Hali ya Hewa (TMA), kutangaza uwezekano wa kunyesha kwa mvua hiyo na kusababisha madhara hasa kwa wananchi waishio katika maeneo hatarishi.

“Ndugu zangu kama tunavyo endelea kuhimizwa na mamlaka ya hali ya hewa, tunatarajia kuwa na mvua nyingi mwaka huu, kwa hiyo niendelee kusisitiza tuchukue tahadhari kwa kuweka mazingira wezeshi kwa kipindi hicho ili kujiepusha na athari zake,” alisema Gugu.

Katika ziara yake, Gugu alitembelea miradi mbalimbali ya maendeleo, ikiwemo ujenzi wa ofisi ya Halmashauri ya Kongwa, unaotekelezwa na Shirika la Uzalishaji Mali la JKT, ambapo alionyesha kutoridhishwa na kasi ya ujenzi wake na kuagiza wahusika kuongeza juhudi ili ukamilike kwa wakati.

“Fanyeni jitihada Kadri inavyo wezekana kulipa siku zilizo Chelewa kwa kuimarisha na kuongeza ufanisi ili kazi iweze kukamilika kwa wakati muafaka,” alisema Gugu.

Aidha, Gogo alikagua ujenzi wa shule mpya ya sekondari katika Kijiji cha Manungu, unaotekelezwa kwa fedha za mradi wa kuboresha elimu ya sekondari (SEQUIP) na kuwapongeza watekelezaji wake kwa kufikia asilimia 95.

Kwa Upande wake, Mkurungezi wa Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa, Dk. Omary Nkullo amesema halmashauri hiyo inaendelea kufanya majukumu yake kwa ufanisi unaotakiwa ili kutoangusha dhamira na jitihada za Serikali.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

Hukumu mahakama kuu yabatilishwa kesi State Oil, Equity Bank Tz

Spread the loveMAHAKAMA ya Rufani, jijini Dar es Salaam, imebatilisha hukumu iliyotolewa...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Geita, Mwanza waongoza kwa mbwa

Spread the loveNaibu waziri wa Mifugo na Uvuvi, Alexander Mnyeti amesema taarifa...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Watumishi 25,039, taasisi 65 wahamia Dodoma

Spread the loveSerikali imesema hadi sasa, jumla ya watumishi 25,039 kutoka Serikali...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB yapata idhini kuwa wakala wa madalali wa DSE

Spread the loveBenki ya NMB imepata idhini kutoka Benki Kuu ya Tanzania...

error: Content is protected !!