JUMLA ya watendaji 18 wa kata, 92 wa vijiji katika Halmashauri ya Wilaya ya Msalala mkoani Shinyanga wanatarajiwa kupatiwa mafunzo maalumu kuhusu matumizi ya Mfumo wa uhasibu na utoaji taarifa za fedha (FFARS) kwa lengo la kuongesa kasi ya ukusanyaji mapato.
Mafunzo hayo ya siku mbili, yamefunguliwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Msalala, Khamis Katimba. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).
Akizungumza wakati akifungua mafunzo hayo Katimba amewataka watendaji hao kusimamia vyema suala la ukusanyaji wa mapato katika maeneo yao.
“Watendaji wenzangu mpo hapa kupata mafunzo ya mfumo wa FFARS lakini niwaombe nendeni mkakusanye mapato, simamieni vyema hilo suala kwani ndiyo uti wa mgongo wa shughuli zote za serikali katika maeneo yenu, hatuwezi kutekeleza shughuli yeyote kama hatuwezi kukusanya mapato. Simamieni kila kinachotakiwa kulipwa kiliipwe na msioneee watu tendeni haki” amesema Ndugu Katimba.
Aidha, katika hatua nyingine Katimba amewataka watendaji hao kudumisha upendo miongoni mwa watumishi kwani wao ndio wasimamizi wakuu wa watumishi katika maeneo yao na hivyo wanapaswa kuonesha dira nzuri kwa watumishi wengine wanaowaongoza.
Nao baadhi ya watendaji wa kata na vijiji waliohudhuria mafunzo hayo wamempongeza Mkurugenzi huyo kwa kuendelea kufanya jitihada kubwa katika kuimarisha ukusanyaji wa mapato ndani ya Halmashauri huku pia wakimshukuru kwa kuendelea kuwa nao karibu na kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili.
Good japo hatujapata details za kilichofundishwa.