AJALI ya meli iliyotokea karibu na nchi ya Italia kwenye kisiwa cha Lampedusa imesababisha vifo vya wahamiaji 41 huku wachache wakinusurika katika ajali hiyo. Anaripoti Mlelwa Kiwale, TUDARCo kwa msaada wa Mitandao ya Kimataifa … (endelea).
Manusura hao waliotoa ushuhuda wao kwenye ajali hiyo katika vyombo vya habari nchini humo, walikuwa kwenye boti iliyokuwa ikitokea nchini Tunisia jijini Sfax na kuelekea Italia ndipo boti hiyo ikazama.
Wahamiaji hao wanne walionusurika, walikuwa siyo wakazi wa Lampedusa bali ni watu wenye asili ya kutoka Guinea na Ivory Coast.
Aidha, taarifa zinaeleza kuwa wahamiaji haramu huwa wanapitia katika lango maarufu la bandari lililo karibu na Lampedusa kwa lengo la kutafuta maisha yaliyo mazuri nchini humo.
Pia vikundi vya uokoaji na boti za doria za Italia zimekuwa zikitoa msaada na kuokoa watu takribani 2,000 ambao walifikia nchini humo.
Hata hivyo, unaelezwa watu 1,800 waliovuka kutoka Afrika Kaskazini na kuelekea Ulaya wamepoteza maisha ndani ya mwaka huu.
Leave a comment