Saturday , 9 December 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Watatu wachukua fomu za urais Tanzani
Habari za Siasa

Watatu wachukua fomu za urais Tanzani

Mutamwega Bati Mgaiwa wa SAU
Spread the love

WAGOMBEA watatu wamechukua fomu ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kugombea Urais wa Tanzania katika Uchaguzi Mkuu wa tarehe 28 Oktoba 2020. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Wagombea hao wamekabidhiwa fomu hizo leo Jumatano tarehe 5 Agosti 2020 na Jaji Semistocles Kaijage, Mwenyekiti wa NEC katika ofisi za tume hiyo zilizoko Ndejengwa jijini Dodoma.

Waliochukua fomu ni, Seif Maalim Seif wa Chama cha Alliance for African Farmers Party (AAFP), aliyeambatana na mgombea Mwenza, Rashid Ligania Rai.

Philipo John Fumbo wa Chama cha Democratic Party (DP) na Leopold Mahona wa Chama cha National Reconstruction Alliance (NRA), aliyeambatana na Mgombea Mwenza Hamis Alli Hassan.

         Soma zaidi:-

Wagombea hao wamechukua fomu hiyo siku ya kwanza baada ya zoezi hilo kufunguliwa leo. Zoezi hilo litafungwa tarehe 25 Agosti 2020.

Akizungumza baada ya kuwakabidhi fomu hiyo, Jaji Kaijage amewataka wagombea hao kurejesha fomu kwa wakati husika kwa ajili ya kupisha zoezi la uteuzi wa wagombea Urais wa Tanzania katika uchaguzi huo.

“Itakapofika siku ya uteuzi tarehe 25 Agosti, 2020 mtarejesha fomu zenu hapa Tume na Tume baada ya kujiridhisha kuwa mnazo sifa itafanya uteuzi,” amesema

Jaji Kaijage amewapongeza wagombea hao kwa kuchukua fomu, akisema kwamba ushiriki wao utachangia kudumisha demokrasia nchini.

“Ninawapongeza kwa kutumia haki yenu ya kikatiba ya kuchagua na kuchaguliwa. Ushiriki wenu utachangia kudumisha demokrasia nchini mwetu na ninawatakia kila la heri,” amesema Jaji Kaijage.

Kesho Alhamisi, Rais John Magufuli, Mgombea wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) atakwenda kuchukua fomu hizo huku Jumamosi tarehe 8 Agosti, 2020, mgombea wa Chadema, Tundu Lissu atakwenda kuchukua fomu.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Mbowe: Miaka 62 ya uhuru tujenge upya mioyo yetu

Spread the loveWAKATI Tanganyika ikiadhimisha miaka 62 tangu kupata uhuru, Mwenyekiti wa...

Habari za Siasa

Rais Samia asamehe wafungwa 2,244

Spread the loveRAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amewasamehe wafungwa 2,244, huku akiwabadilishia...

Habari za SiasaTangulizi

Rais Samia ataka jamii inayohoji mafisadi

Spread the loveRAIS Samia Suluhu Hassan ametoa maagizo juu ya uboreshaji dira...

Habari za SiasaTangulizi

Kapinga: Kukatika kwa umeme siyo hujuma

Spread the loveNaibu Waziri wa Nishati, Judith Kapinga amesema Serikali ipo kazini...

error: Content is protected !!