Tuesday , 26 September 2023
Home Habari Mchanganyiko Watafiti wasisitizwa ushiriki jopo la kimataifa la sayansi ya mabadiliko ya hali ya hewa
Habari Mchanganyiko

Watafiti wasisitizwa ushiriki jopo la kimataifa la sayansi ya mabadiliko ya hali ya hewa

Spread the love

 

KAIMU Mkurugenzi Mkuu, Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) na Makamu Mwenyekiti wa Jopo la Kimataifa la Sayansi ya Mabadiliko ya Hali ya Hewa na Tabianchi, Dkt. Ladislaus Chang’a amewasisitiza watafiti mbalimbali nchini kutumia fursa zilizopo katika Jopo hilo kwa kushiriki kikamilifu na kutoa mchango wa sayansi ya mabadiliko ya hali ya hewa ngazi ya nchi. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Dk. Chang’a alisema hayo wakati akizungumza na wanasayansi, watafiti, viongozi na watumishi kutoka Idara mbalimbali za Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) ikiwa ni moja ya mkakati wa kuhimiza na kuongeza mchango wa nchi za Afrika kwenye ripoti mbalimbali zinazotolewa na Jopo hilo la Kimataifa.

“Huu ni mkutano wangu wa kwanza kama Makamu Mwenyekiti wa IPCC nikiwa na jukumu la kuhamasisha ushiriki wa Afrika katika mchakato na kazi za IPCC, ikiwemo maandalizi ya Ripoti ya Saba.

“Viongozi wa sasa wa IPCC kutoka Afrika tumejipa jukumu la kuhamasisha na kuhakikisha ongezeko la ushiriki wa watafiti kutoka Afrika katika Jopo la IPCC. Aidha, niwajulishe kuwa mchakato wa ripoti hiyo, unatarajiwa kuanza hivi karibuni,” alisema Dk. Chang’a.

Naye, Mkurugenzi wa Taasisi ya Tathmini Rasilimali, UDSM Prof. Joel Kirway alimpongeza Dkt. Chang’a kwa kuchaguliwa kuwa Makamu Mwenyekiti wa IPCC na kuitikia mwaliko wa kukutana na watumishi mbalimbali wa UDSM ili kuwasilisha mada ya fursa zilizopo katika Jopo la IPCC kwa Chuo cha Dar es Salaam ambacho kina Kituo cha Taaluma za Mabadiliko ya Tabianchi, kwa kutambua mchango katika maendeleo ya nchi na Afrika kwa ujumla. Aidha, baada ya majadiliano ya kina, Prof. aliahidi kutoa ushirikiano kwa kushirikisha idadi kubwa ya watumishi na wanachuo ili kuleta mabadiliko chanya katika machapisho mbalimbali ya IPCC.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Rais Samia apewa tano ujenzi barabara Mtwara

Spread the loveWANANCHI wa Mkoa wa Mtwara, wameishukuru Serikali ya Rais Dk....

BiasharaHabari Mchanganyiko

Serikali kununua mitambo 15 ya kuchoronga miamba

Spread the loveSerikali kupitia Wizara ya Madini imepanga kununua mitambo 15 ya...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Mtanzania aweka rekodi kimataifa kwa kiwanda cha kusafisha dhahabu

Spread the loveIMEELEZWA kuwa Kiwanda cha Kusafisha dhahabu cha Geita Gold Refinery...

Habari Mchanganyiko

MAIPAC kusaidia Kompyuta shule ya Arusha Alliance

Spread the loveTaasisi ya Wanahabari ya kusaidia Jamii za pembezoni (MAIPAC) imeahidi...

error: Content is protected !!