Friday , 17 May 2024
Home Habari Mchanganyiko OMUKA HUB, NDI wafanikisha majadiliano Jukwaa la wanawake katika siasa
Habari Mchanganyiko

OMUKA HUB, NDI wafanikisha majadiliano Jukwaa la wanawake katika siasa

Spread the love

SHIRIKA la Omuka Hub ambalo kwa kushirikiana na Shirika la Kimataifa la Marekani National Democratic Institute – (NDI) wameandaa majadiliano kwa Jukwaa la Wanawake katika Siasa, kujadili mapendekezo ya Kikosi Kazi na Maazimio ya Mkutano Maalum wa Baraza la Vyama Vya Siasa uliofanyika tarehe 11 hadi 13 Septemba 2023 mkoani Dar es Salaam. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Majadiliano hayo yameandaliwa chini ya uratibu wa Mbunge wa Viti Maalum, Neema Lugangira ambapo amesema lengo ni kumuunga mkono maono ya Rais Samia Suluhu Hassan katika kuimarisha uwakilishi wa wanawake kwenye siasa.

“Mjadala juu ya ushiriki wa wanawake katika siasa katika ngazi zote kuanzia kitongoji hadi Taifa umefanyika Bukoba, Mjini na umehudhuriwa na washiriki 100 kutoka makundi mbalimbali ya jamii ikiwemo viongozi wa dini, siasa, wakina mama viongozi , wakuu wa mashirika/NGOs na wengine.

Lugangira amesema maazimio ya mjadala huo yanakwenda kuwa chachu katika utekelezaji wa maono ya Rais Samia ya kuimarisha uwakilishi wa wanawake katika siasa.

Aidha, amesema maazimio hayo yatawasilishwa kwa ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, kupitia Msajili Msaidizi, Sisty Nyahoza, ambaye alikuwa mgeni rasmi katika semina hiyo.

“Washiriki wa semina hii wamempongeza Rais Samia kwa hotuba nzuri aliyotoa wakati anafungua Mkutano Maalum wa Baraza la Vyama Vya Siasa kwani imeeleza uhalisia na inatoa dira jinsi ambavyo shughuli za siasa zinapaswa kufanyika nchini ili kudumisha amani, utulivu na umoja wa kitaifa,” amesema.

Mbunge huyo ambaye amejipambanua katika kuinua wananchi wa kada mbalimbali amesema washiriki wamempongeza Rais Samia katika kuongoza nchi, hasa kwa kuanza kutekeleza map anayoiongoza kwa kutekeleza sehemu kubwa ya mapendekezo ya Kikosi Kazi.

Lugangira amesema washiriki wa semina hiyo wameridhishwa na maazimio ya washiriki wa mkutano maalum ulioandaliwa na Baraza la Vyama vya Siasa na Ofisi ya Msajili.

Kwa upande wake Msajili Msaidizi, Nyahoza amempongeza Mbunge Lugangira kwa ubunifu wake mkubwa wa kuandaa majadiliano hayo ambayo yamehusishaa Jukwaa la Wanawake katika Siasa kwa lengo la kujadili utekelezaji wa Mapendekezo ya Kikosi Kazi na Maazimio ya Mkutano Maalum wa Baraza la Vyama Vya Siasa katika ngazi ya jamii.

Nyahoza amewapongeza washiriki kwa mjadala mzuri na amechukua maoni yao ambayo yatafanyiwa kazi.

“Kikubwa zaidi nimefurahia kukutana na washiriki kutoka ngazi ya jamii ambao wameonesha uelewa mkubwa na masuala ya ushiriki wa wanawake katika siasa,” amesema.

Msajili Msaidizi Nyahoza ametumia nafasi hiyo kuliomba Shirika la NDI kuendelea kushirikiana na Mwanziishi wa Shirika la Umuka Hub ili mafunzo hayo yafike kila kona ya nchi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Udhibiti wa serikali wakera asasi za kiraia

Spread the loveBaadhi ya wadau wa demokrasia na viongozi wa asasi za...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Nape aomba bajeti ‘kiduchu’ kwa mwaka 2024/25

Spread the loveWaziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Seneta: Wanasiasa hawasaidii mchakato wa Katiba mpya

Spread the loveSeneta wa jimbo la Busia, nchini Kenya, Okiya Okoiti Andrew...

Habari Mchanganyiko

Wananchi washauriwa kuongeza uelewa wa kujikinga na majanga

Spread the love WITO umetolewa kwa wananchi kuongeza uelewa na utayari kabla...

error: Content is protected !!