Saturday , 27 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Wanawake Ubungo waandamana hadi kwa DC kudai maji
Habari Mchanganyiko

Wanawake Ubungo waandamana hadi kwa DC kudai maji

Spread the love

WANAWAKE kadhaa wa Kata ya Luguruni wameandamana hadi ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Herry James, wakidai kutopata huduma ya maji kwa miezi mitatu sasa. Anaripoti Mwandishi Wetu Dar es Salaam … (endelea)

Akina mama hao wameandamana wakiwa na ndoo tupu kichani huku wakiimba nyimbo za wito kwa Rais Samia Suluhu Hassan, Mkuu wa Wilaya na Mwenyekiti kuwatua ndoo hizo kichwani.

Mara baada ya kuapishwa kuwa Rais wa awamu ya sita, Rais Samia aliahidi kuwatua akina mama ndoo kichwani na kuongeza bajeti ya maji karibu mara mbili ili kufanikisha azma hiyo.

Kheri James, Mkuu wilaya ya Ubungo

Hata hivyo kutokana na ukame ulio yakumba maeneo mengi ya nchi, mito inayotegemewa kuzalisha maji imekauka na kusababisha uhaba mkubwa wa maji.

Mkuu wa Wilaya hiyo James, amewahakikishia wanawake hao kuwa maji yatatoka hii leo kufikia majira ya saa 7 na kuziagiza mamalak za maji kuzingatia ratiba ya mgawo wa maji.

Ameonya kuwa wananchi wanakosa maji ilihali maeneo mengine maji yanamwagika barabarani kutokana na ubovu wa miundombinu.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Wakili: Ukimpa zawadi mwenza marufuku kumpora hata mkiachana

Spread the love  WANANDOA na watu waliko kwenye mahusiano ya kimapenzi, wamekumbushwa...

Habari Mchanganyiko

Majaliwa: Mvua zimesababisha vifo vya watu 155, kuendelea hadi Mei

Spread the love  WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amesema mvua kubwa za El-Nino...

Habari Mchanganyiko

Exim Bank yatoa  vitanda kwa shule ya Jeshi la Polisi Moshi

Spread the love  BENKI ya Exim imekabidhii  seti ya vitanda kwa Shule...

Habari Mchanganyiko

NBC yakabidhi vitanda Shule ya Polisi Moshi

Spread the loveBenki ya NBC imekabidhi msaada wa vitanda 28 kwa Shule...

error: Content is protected !!