October 6, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Wananchi wamng’oa Rais Bolvia

Wananchi Bolivia wakiandamana

Spread the love

EVO Morales, Rais wa Bolvia amejiuzulu ili kupunguza ghasia zilizotokana na maandamano ya kupinga matokeo ya uchaguzi, yaliyomuweka madarakani. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa…(endelea).

Morales ametangaza uamuzi huo jana tarehe 11 Novemba 2019, huku akionesha hofu ya kukamatwa, kufuatia maandamano hayo.

Maandamano hayo yalianza wiki kadhaa zilizopita, baada ya uchaguzi wa urais kufanyika tarehe 20 Oktoba mwaka huu.

Katika video fupi inaonesha raia wa Bolvia wakiandamana katika mitaa ya mji wa La Paz, huku Jeshi la nchi hiyo likimtaka ajiuzulu.

Morales aliyeiongoza Bolvia kwa takribani miaka 14, amesema atawasilisha barua ya kujiuzulu bungeni, ili kurejesha hali ya utulivu nchini humo

error: Content is protected !!