December 3, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mdee atinga bungeni, Spika Ndugai ‘amaindi’

Spread the love

UNAWEZA kujiuliza, kuna kitu gani kilichopo kati ya Halima Mdee, Mbunge wa Kawe na Job Ndugai, Spika wa Bunge? Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma…(endelea).

Leo tarehe 11 Novemba 2019, Mdee amerejea bungeni baada ya kusimamishwa kwa mikutano miwili, kutokana na kuunga mkono kauli ya aliyekuwa Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), kuwa Bunge ni dhaifu.

Mdee aliwasili bungeni wakati kikao kinaendelea, ambapo Hussein Bashe, Naibu Waziri wa Kilimo akiwa anaongeza, kuwasili kwake kuliamsha shangwe kwa wabunge wa upinzani huku wakipiga meza ‘kumlaki’ mbunge huyo.

Kutokana na shamra hizo, Waziri Bashe alilazimika kusitisha kile alichokuwa akizungumza huku Mdee akiwapungua mkono kuashiria salamu na kuitikia mapekezi hayo.

Kwa makofi hayo, Spika Ndugai aliwaambia wabunge hao kwamba, wanaweza kumponza na kwamba ‘si wanamjua’.

“Tulieni, hizo kelele zinaweza kumponza mwenzenu, ohoo! si mnanijua, sitanii..,” amesema Spika Ndugai.

error: Content is protected !!