Friday , 26 April 2024
Home Kitengo Maisha Afya Wakuu wa mikoa wapewa maagizo tahadhari ya Ebola
AfyaTangulizi

Wakuu wa mikoa wapewa maagizo tahadhari ya Ebola

Ummy Mwalimu
Spread the love

WAZIRI wa Afya Ummy Mwalimu ametoa tahadhari ya ugonjwa wa Ebola na kuagiza wakuu wote wa mikoa kujiandaa endapo itatokea kisa chochote au kifo kitakachosababishwa na virusi hao. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Maagizo hayo ameyatoa leo Jumatano tarehe 28 Septemba, 2022, wakati akitoa taarifa kuhusu hali ya ugonjwa huo ambao tayari umeua watu kadhaa na wengine kuambukizwa katika nchi jirani ya Uganda.

“Nawaagiza wakuu wa mikoa kote nchini kila mkoa kujiandaa na ni lazima waainishe ni gari lipi la wagonjwa ‘ambulance’ itatumika, timu ya wataalamu wa afua, mtu wa maabara ni yupi na mgonjwa akipatikana anapelekwa wapi, kuhakikisha kuna vifaa na atapelekwa wapi,” amesema Mwalimu.

Amewataka kutodharau tetesi yeyote kuhusiana na ugonjwa huo na kuwataka kuandaa maeneo ya mazishi endapo mgonjwa wa Ebola ata[poteza maisha.

Pia ametoa wito kwa jamii kusitisha safari zote hasa kwenda nchini Uganda, kuepeuka kutembea maeneo hatarishi yenye ugonjwa, kuacha kula nyama ambayo haijapikwa vizuri, kuepuka kugusa mate, machozi na kunawa mikono mara kwa mara kwa maji tiririka na sabuni.

 

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Afya

Mloganzila yajipanga kupandikizaji wa ini

Spread the love  HOSPITALI ya Taifa Muhimbili-Mloganzila imesema kutokana na uwekezaji uliofanywa...

Habari za SiasaTangulizi

Biteko ataja vipaumbele 7 bajeti nishati 2024/25

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

Habari za SiasaTangulizi

Mpwa wa Magufuli mbaroni kwa kusambaza picha za utupu

Spread the loveJESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewakamata...

Habari za SiasaTangulizi

Shibuda amlima waraka mzito Bulembo

Spread the loveMKONGWE wa siasa nchini, John Shibuda amemshukia kada maarufu wa...

error: Content is protected !!