Saturday , 27 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Wakili Mwabukusi mbaroni, yumo pia Masonga na Mdude
Habari za SiasaTangulizi

Wakili Mwabukusi mbaroni, yumo pia Masonga na Mdude

Spread the love

MWANASHERIA mahiri nchini na Wakili wa kujitegemea, Boniface Mwabukusi amekamatwa na jeshi la Polisi. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).

Taarifa kutoka vyanzo mbalimbali, akiwamo Askofu Emmaus Mwamakula zinasema, Mwabukusi amekamatwa katika maeneo ya Mikumi, mkoani Morogoro. Anatuhumiwa kwa uchochezi.

Mwabukusi alikuwa mmoja wa wanasheria waliofungua kesi ya kupinga mkataba uliofungwa kati ya serikali na Dubai.

Mdude Nyagali

 Kukamatwa kwa Mwabukusi  kumekuja muda mfupi baada ya Mkuu wa Jeshi la Polisi kuutangazia ulimwengu, kwamba “kuna njama za kumuangusha Rais wa Jamhuri, Dk. Samia Suluhu Hassan.”

Akiandika kupitia mtandao wake wa kijamii, Askofu Mwamakula anasema,

“Taarifa zilizotufikia hivi punde ni kuwa wakili msomi Boniface Kanjunjule Mwabukusi, amekamatwa na Jeshi la Polisi kule Mikumi, Morogoro akiwa pamoja na Katibu wa Kanda wa CHADEMA, Emmanuel Masonga.

“Walikuwa safarini kuelekea Dar es Salaam pamoja na Mdude ndipo wakazuiwa Mikumi.

“Alikamatwa Mdude saa 10 usiku na baadaye maelekezo yakaja ya kukamatwa na wao pia. Mwabukusi ametujulisha kwa simu kuwa wao wameelezwa wamekamatwa kwa tuhuma za uchochezi na simu zao zimechukuliwa.

“Wakili Mwabukusi ndiye aliyesimamia kesi ya kupinga mkataba wa Bandari iliyofunguliwa Mahakama Kuu Kanda ya Mbeya.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

ACT: Waongoza watalii wapate maslahi yao inavyostahili

Spread the loveCHAMA cha ACT-Wazalendo kimeitaka serikali kuhakikisha inasimamia maslahi stahiki ya...

Habari za SiasaTangulizi

Prof. Lipumba ajitosa kuviunganisha vyama vya siasa Burundi

Spread the love  MWENYEKITI wa Kituo Cha Demokrasia Tanzania (TCD), Prof. Ibrahim...

Habari za SiasaTangulizi

Samia awataka watanzania kudumisha muungano

Spread the loveRais wa Tanzania,Samia Suluhu Hassan amewataka Watanzania kuendeleza Muungano kwa...

Habari za Siasa

Prof. Muhongo akomalia matumizi nishati jadidifu kuondoa uhaba wa umeme

Spread the love  MBUNGE wa Musoma Vijijini (CCM), Profesa Sospeter Muhongo, ameendelea...

error: Content is protected !!