Friday , 3 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Wafanyabishara washauriwa kutumia kituo jumuishi
Habari Mchanganyiko

Wafanyabishara washauriwa kutumia kituo jumuishi

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Utumishi, Jenista Mhagama
Spread the love

 

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Jenista Mhagama amewashauri na kuwataka wafanyabiashara wadogowadogo mkoani Arusha kutumia Kituo Jumuishi cha Urasimishaji na Uendelezaji wa Biashara ambacho kimeanzishwa na mpango wa kurasimisha rasilimali na biashara kwa kushirikiana na jiji la Arusha. Anaripoti Queen Lema, Arusha … (endelea). 

Aidha lengo halisi ni kuhakikisha kuwa biashara za wafanyabiashara hao pamoja na pato la taifa linakuwa kwa kiwango kikubwa sana.

Mhagama aliyasema jijini Arusha wakati akizindua kituo cha urasimishaji  kilichopo katika kata ya Kati, Mtaa wa Pangani jijini hapo.

Alisema lengo halisi la Serikali ni kuhakikisha kuwa kila mara kuna kuwa na mikakati ya kuweza kuwasaidia wafanyabiashara ambapo sasa kupitia kituo hicho wataweza kupata msaada na ufafanuzi juu ya masuala mbalimbali.

“Kituo hiki kimeanzishwa mahususi kwa ajili ya kuwasaidia wajasiriamali kujifunza mambo mbalimbali pamoja na kupatiwa mbinu tofauti za kibiashara, hivyo ni fursa kwao kukitembelea ili kupata huduma hiyo.

Lakini pia kituo kitasaidia kurasimisha biashara zenu na kuweza kutambulika na taasisi za kifedha ili muweze kupata mikopo katika taasisi hizo kwa lengo la kuinua biashara zenu kwa maendeleo yenu binafsi na taifa kwa ujumla,”  Jenista amesisitiza

Katika  hatua nyingine  waziri huyo aliwataka wajasiriamali wa Arusha kuhakikisha wanapata  huduma bora katika kituo hicho, sanjari na taasisi zote zinazotoa huduma jumuishi kushiriki kikamilifu kutoa huduma, ili wafanyabiashara hao wasipate au kukutana na changamoto mbalimbali pindi  wanapoenda kupata huduma katika kituo hicho.

Nasisitiza kwa mara nyingine kuwa kupitia mpango wa  MKURABITA  sisi kama Serikali tumeweza fedha nyingi kuanzisha kituo hichi ambacho ni kikubwa chenye ubora, hivyo taasisi zote jumuishi zinatakiwa zitoe huduma na kuondoa kadhia kwa wafanyabiashara hao kwa kuwapatia huduma inayostahili kama ilivyokusudiwa,” Mhe. Jenista amesisitiza.

Awali , Mratibu wa MKURABITA, Dk Seraphia Mgembe alisema kuwa bado wana mikakati mbalimbali ambayo wataweza  kushirikiana na Halmashauri ya Jiji la Arusha katika mambo mbalimbali ya kuwawezesha wafanyabiashara hao waweze kujikwamua kiuchumi.

Alitaja mkakati huo kuwa ni pamoja na kuratibu mafunzo ambayo yataweza kuwapa uelewa juu ya biashara zao.

Kituo Jumuishi cha Urasimishaji na Uendelezaji wa Biashara kimeanzishwa ili kuwasaidia na kuwarahisishia wafanyabiashara wa Jiji la Arusha kupata huduma zote za ushauri wa biashara pamoja na kupata mahitaji yote ya kibiashara katika sehemu moja.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

Wafanyakazi waidai STAMICO mishahara ya bilioni 1

Spread the loveWALIOKUWA wafanyakazi wa mgodi wa Shirika la Madini la Taifa...

AfyaHabari Mchanganyiko

200 wapimwa afya na GGML katika maonesho ya OSHA

Spread the loveZAIDI ya watu 200 jijini Arusha wamejitokeza kupimwa afya na...

Habari Mchanganyiko

Mfanyakazi CRDB atoa sababu za kubambikiwa kesi, hukumu Mei 30

Spread the love  MFANYAKAZI wa Benki ya CRDB, Ibrahim Masahi (40) ameieleza...

Habari Mchanganyiko

Waziri Ummy atangaza Tanzania kuwa kitovu cha utalii tiba

Spread the loveSERIKALI imesema imedhamiria kuifanya Tanzania kuwa kitovu cha matibabu ya...

error: Content is protected !!