Friday , 3 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Wadau wa habari wawaangukia wabunge
Habari Mchanganyiko

Wadau wa habari wawaangukia wabunge

Deudatus Balile, Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri (TEF)
Spread the love

 

WADAU wa Haki ya Kupata Taarifa nchini (CoRI), wamewaomba wabunge kuwasikiliza waandishi wa habari ili wapate mapendekezo yao yaliyoachwa katika Muswada wa Mabadiliko ya Sheria ya Habari, kwa ajili ya kuyawasilisha bungeni ili yaingizwe katika marekebisho hayo. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Wito huo umetolewa leo Alhamisi, tarehe 20 Aprili 2023, wakati wadau hao walipokutana jijini Dar es Salaam, kwa ajili ya kupitia muswada huo uliowasilishwa bungeni jijini Dodoma, tarehe 10 Februari mwaka huu.

Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Deodatus Balile, amesema wadau wa habari watazungumza na wabunge kuhusu athari zinazoweza kuifika tasnia hiyo kutokana na vifungu vilivyomo kwenye Sheria ya Huduma ya Vyombo vya Habari ya 2016, pamoja na muswada marekebisho yake, ili wawasaidie kupaza sauti wakianza kujadili bungeni.

“Tutakwenda kuzungumza na wabunge kuhusu athari zinazoweza kuifika tasnia ya habari kutokana na baadhi ya vifungu vilivyomo kwenye sheria na marekebisho yaliyofanywa na serikali ili watusaidie kurekebisha siku wakianza kujadili bungeni,” amesema Balile.

Balile amesema, miongoni mwa kifungu ambacho wanataka kifanyiwe marekebisho na kimeachwa kama kilivyo kwenye muswada huo, ni cha tisa ambacho kinampa mamlaka Mkurugenzi wa Habari (Maelezo) kutoa leseni ya kuchapisha gazeti.

Kwa upande wake Mjumbe wa kamati ya Utendaji ya TEF, Nevil Meena ameishukuru Serikali kwa kukubali kurekebisha sheria hiyo, huku akisema muswada huo kama usipoboreshwa zaidi kwa kuingiza baadhi ya mapendekezo yaliyoachwa, wadau wa habari hawataweza kufanya kazi kwa uhuru.

“Lakini sheria ikibaki kama ilivyopendekezwa kwenye muswada ule, hatuwezi kufanya kazi kwa uhuru na weledi tuliokusudia. Hatususi kwa kile kilichopelekwa, tutaendelea kushawishi kuda mabadiliko ten ana tena. Mchakato wa sheria ni wa kuendelea, tukiotoka sisi watakuja wengine kuendeleza tulipoishia,” amesema Meena.

Naye Rose Mwalongo, kutoka Taasisi ya Vyombo vya Habari kwa Maendeleo ya Jamii (TAMCOTE), amesema ni vyema mapendekezo ya wadau wa habari yaliyotolewa juu ya uboreshaji sheria hiyo yangeizwa katika muswada huo, ili mambo yanayolalamikiwa kuminya uhuru wa habari yaondolewe, ikiwemo sharti la magazeti kukata leseni kila mwaka.

Deus Kibamba, Mjumbe wa CoRI amesema “muswada huu ambao serikali imeupeleka bungeni, una mambo mazuri lakini ni machache, mengi bado hayaingizwa. Tunaomba wabunge wajue kuwa kuna mambo mengine zaidi ya habari ambayo tumependekeza, tunaomba yaingie kwa lengo lille ile la kuimarisha tasnia ya habari.”

James Marenga, Makamu Mwenyekiti wa Misa-Tan , amesema sheria ina upungufu ambao unapaswa upigiwe kelele na ufanyiwe marekebisho ili sekta ya habari ikue zaidi.

Amesema mapendekezo ya sheria yaliyotolewa na Serikali ni maeneo tisa tu kati ya 21 yaliyopendekezwa yafanyiwe marekebisho na Serikali.

Amesema miongoni mwa mapendekezo yaliyofanyiwa kazi na Serikali na wanaunga mkono kifungu cha 5 (1) kwa kumuondoa Mkurugenzi wa Habari Maelezo kuwa mratibu wa matangazo kwa vyombo vya habari.

“Kifungu 38 kinachozungumzia kashfa ambavyo awali ilionekana ni jinai nacho kimefanyiwa marekebisho lakini mengi ni kupunguzwa kwa makosa na adhabu zake badala ya kuondoa” amesema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

Wafanyakazi waidai STAMICO mishahara ya bilioni 1

Spread the loveWALIOKUWA wafanyakazi wa mgodi wa Shirika la Madini la Taifa...

AfyaHabari Mchanganyiko

200 wapimwa afya na GGML katika maonesho ya OSHA

Spread the loveZAIDI ya watu 200 jijini Arusha wamejitokeza kupimwa afya na...

Habari Mchanganyiko

Mfanyakazi CRDB atoa sababu za kubambikiwa kesi, hukumu Mei 30

Spread the love  MFANYAKAZI wa Benki ya CRDB, Ibrahim Masahi (40) ameieleza...

Habari Mchanganyiko

Waziri Ummy atangaza Tanzania kuwa kitovu cha utalii tiba

Spread the loveSERIKALI imesema imedhamiria kuifanya Tanzania kuwa kitovu cha matibabu ya...

error: Content is protected !!