Saturday , 9 December 2023
Home Habari Mchanganyiko Wachina wakutwa na hatia, watoa faini
Habari Mchanganyiko

Wachina wakutwa na hatia, watoa faini

Zheng Rongman (50) (kushoto) na Ou Ya (47)
Spread the love

MAHAKAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam imewahukumu raia wawili wa China, Zheng Rongman (50) na Ou Ya (47), kulipa faini ya Sh 1milioni kila mmoja, baada ya kupatikana na hatia ya kutoa rushwa. Anaripoti Faki Sosi, Dar es Salaam … (endelea).

Rongman ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Ronglan International Industry  and Trade Co. Ltd.

Akitoa hukumu hiyo, Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakamani hiyo, Huruma Shaidi amesema, mahakama hiyo imetaifisha fedha kiasi cha Sh 11.5 milioni na kuwa mali ya serikali.

Hakimu Shaidi amesema, washtakiwa wametiwa hatiani kama walivyoshtakiwa.

“Mahakama hii inawahuku kila mmoja kulipa faini ya Sh 1 milioni na kiasi cha Dola za Marekani 5,000 ambapo ni sawa na Sh 11.5 milioni zimetaifishwa na kuwa mali ya serikali,” amesema Hakimu Shaidi.

Hakimu Shaidi ameeleza, wawekezaji wote wanatakiwa wafuate sheria na taratibu zilizopo nchini, hivyo kosa walilofanya washtakiwa hao halikubaliki.

Awali, wakili anayewatetea washtakiwa hao, Steven Bwana akisaidiana na Peter Lyimo na Denis Mdoe, ameomba mahakama iwapunguzie adhabu.

Bwana amedai, washtakiwa hao ni kosa lao la kwanza na kupitia kampuni yao, wameweza kutoa ajira kwa Watanzania 100 na wana familia inayowategemea.

Akisoma maelezo ya washtakiwa, wakili kutoka Takukuru, Ipyana Mwakatobe alidai mahakamani hapo, kesi hiyo iliitwa kwa ajili ya kuwasomea maelezo ya awali.

Amedia tarehe 24 Februari 2020, washtakiwa hao walifika Makao Makuu ya Mamlaka ya Mapato nchini (TRA), yaliyopo Wilaya ya Ilala jijini humo kwa ajili ya kuona na kuonana na Kamishna Mkuu wa TRA, Dk. Edwin Mhende.

Mwakatobe amedai, siku hiyo ya tukio, saa 10:00 jioni washtakiwa hao walionana na Kamishna Mkuu wa TRA, Dk Mhende Ofisi kwake akiwa na msaidizi wake.

Na kwamba, walimueleza wana tatizo na kodi na waliwasilisha nyaraka kadhaa wakidia kuwa, wamekadiriwa kiwango kikubwa cha kodi, hivyo walimuomba kamishna huyo atatue mgogoro huo.

Washtakiwa hao baada ya kumueleza hayo Dk. Mhende, wametoa kitita cha fedha ambazo ni Dola za Marekani 5,000 na kumkabidhi kamishna huyo, kama kishawishi ili aweze kuwasaidia katika suala lao la kodi, ambapo kampuni yao ilipaswa kulipa kodi ya Sh 1.3 bilioni.

Mwakatobe amedai, Dk. Mhende alimuelekeza msaidizi wake kuhesabu fedha hizo alizopewa na washtakiwa hao, na kubaini kuwa zilikuwa ni Dola za Marekani 5,000 ambapo zilikuwa noti 50 za dola mia moja kila mmoja.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Kesi ya mfanyakazi wa CRDB itaendelea J’tatu

Spread the love  MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kinondoni, Dar es Salaam inatarajia...

Habari Mchanganyiko

Mawasiliano Dar – Bagamoyo yarejea

Spread the loveMAWASILIANO ya barabara ya Mkoa wa Pwani na Dar es...

Habari Mchanganyiko

Tanesco: Mvua chanzo kukatika umeme leo

Spread the loveShirika la Umeme Tanzania (TANESCO) limedai kuwa hitilafu iliyojitokeza katika...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Zara tours yajivunia kupandisha wageni 228 Mlima Kilimanjaro

Spread the loveKampuni ya utalii ya Zara tours ya mjini Moshi mkoani...

error: Content is protected !!