October 5, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Wachafukoga marufuku kuingia mjini-Makonda

Spread the love

WATANZANI wachafu wamepigwa marufuku kuonekana mijini hususani katika kipindi hiki cha Mkutano wa Nchi Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC). Anaripoti Faki Sosi … (endelea).

Marufuku hiyo imetolewa na Paul Makonda, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam leo tarehe 29 Julai 2019, kwenye uzinduzi wa kampeni ya usafi wa jiji hilo.

Kampeni hiyo imezinduliwa ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya mkutano huo wa 39. Mkutano huo unatarajiwa kufanyika kwa siku mbili, kuanzia tarehe 18 hadi 19 Agosti 2019.

Makonda amepiga marufuku ya kuingia katika viunga vya mjini na nguo zisizonyooshwa “tabia ya kuna mjini bila kunyoosha nguo ni marufuku,” na kuongeza “tabia ya kuja mjini hujaoga ni aibu.”

Kiongozi huo wa Dar es Salaam pia ameonya watu wenye tabia za kwenda mjini bila kuwa wasafi, na kwamba ni bora wasubiri mkutano huo upite.

“Watu wanatembea tu na chawa, kama huwezi kuwa msafi basi subiri mwezi huu upite…”kama hufui nguo, kama huogi, pumzika kidogo kuja mjini, kwa kipindi hiki tuvumiliane,” amesema.

Katika kampeni hiyo Makonda ameshauri kwamba, dereva yeyote atakayekamatwa anatupa takataka asitozwe faini na badala yake apewe eneo la kufanya usafi.

Kwenye harakati hizo Makonda amesema, anafanya hivyo kwa kuwa hataki kumtia aibu mkuu wa nchi, Rais John Magufuli ambaye ndiye mwenyeji wa mkutano huo.

error: Content is protected !!