August 8, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Wabunge, Spika watoa Sh. 100 milioni kwa wafiwa

Job Ndugai, Spika wa Bunge la Tanzania na Mbunge wa Jimbo la Kongwa

Spread the love

WABUNGE wa bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wameadhimia kutoa milioni 86 pesa za posho ya kikao cha siku kwa ajili ya rambirambi kwa familia za wafiwa, wanafunzi na wafanyakazi wa shule ya msingi Lucky Vincent Academy mkoani Arusha, anaandika Hamisi Mguta.

Job Ndugai, Spika wa Bunge la Tanzania, amesema wabunge wamekubaliana kutoa posho zao za siku ya leo kupeleka kwa familia za wafiwa kama rambirambi zao, marehemu waliopoteza maisha katika ajali mkoani humo.

“Tumekubaliana kwa kauli moja humu bungeni tutoe posho ya siku moja kama rambirambi yetu, posho hiyo tutaipeleka mara moja kwa Mkuu wa Mkoa Mrisho Gambo na itagawiwa sawa sawa kwa wafiwa wote,”amesema Ndugai.

Kiasi cha rambirambi kinachotolewa na Bunge ni Sh. 100 milioni ambapo amefafanua kuwa Sh, 86 milioni zinatokana na posho hizo za kikao cha siku moja na Sh. 14 milioni zimetoka katika Ofisi ya Spika.

Tazama video chini, Job Ndugai akifafanua juu ya rambirambi hizo

error: Content is protected !!