Wednesday , 1 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Waandishi watakiwa kuchangamkia fursa za SADC
Habari Mchanganyiko

Waandishi watakiwa kuchangamkia fursa za SADC

Spread the love

WAANDISHI wa habari nchini wametakiwa kuandika fursa zilizopo katika Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) ili kuvutia wawekezaji, hali ambayo itakuza uchumi wa nchi wanachama. Anaripoti Suleiman Msuya, Dar es Salaam … (endelea).

Kauli hiyo na Mratibu wa Kituo cha Malengo ya Maendeleo Endelevu Afrika (SDGCA), Ambrose Rwaheru wakati akizungumza na waandishi wa habari walioshiriki mafunzo, hivi karibuni jijini Dar es Salaam.

Alisema SDGCA inatekeleza Mradi wa Mpango Jumuishi wa Kujenga Uwezo wa Kitaasisi (IICB) kwa Sekretarieti ya SADC na Wadau wa Kitaifa kwa kushirikiana na wadau wake katika kufikia ahadi za kikanda hususan,

Mpango Elekezi wa Kikanda wa Maendeleo (RISDP) – (2020-2030) na Dira ya 2050 ya SADC.

Rwaheru alisema SDGC limejipanga kutoa mafunzo kwa waandishi wa habari wa nchi husika, ili waweze kuwa na uelewa wa masuala ya SADC, hivyo kuwataka watoe ushirikiano kufikia lengo hilo.

“Nchi za SADC zina fursa nyingi, kama ardhi, madini, misitu na nyingine nyingi ambazo zikielezewa vizuri zitavutia wawekezaji na kuchangia ukuaji wa uchumi na maendeleo kwa nchi na wananchi,” alisema.

Mratibu huyo alisema mradi huo umefadhiliwa na Umoja wa Ulaya (EU) na unatekelezwa katika nchi za Tanzania, Malawi, Zambia na Zimbabwe.

Kwa upande wake Mratibu wa Mtandao wa Wakulima wa Afrika Mashariki na Kusini mwa Afrika (ESAFF), Joe Mzinga, alisema lengo la mafunzo hayo ni kuhakikisha vyombo vya habari vinajengewa uwezo na kuwezeshwa kutoa habari zaidi kuhuszau SADC.

Alisema vyombo vya habari na waandishi wakipatiwa habari za kina kuhusu SADC watasaidia wananchi na wadau wengine kujua fursa zilizopo na kuzifanyia kazi.

“Kuna haja ya kushirikisha vyombo vya habari katika ngazi zote, tafsiri ya taarifa mbalimbali za SADC, ili kuakisi muktadha wa ndani, hivyo imani yangu ni mafunzo haya yawe chachu kwenu kuandika habari za jumuiya hiyo,” alisema.

Mzinga alieleza kuna makundi mbalimbali yanapaswa kushirikishwa katika Jumuiya hiyo ikiwemo mashirika yasiyo ya kiserikali, madhebu ya dini na taasisi zingine na hakuna anayepaswa kuchwa nyuma.

Naye Makamu Mwenyekiti wa Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika (MISA-TAN) Wakili James Marenga aliwaambia waandishi kutafuta taarifa mbalimbali za SADC na kuziandika ili ziweze kufahamika.

Marenga alisema zipo fursa nyingi katika nchi wanachama, hivyo kinachohitajika ni kutolewa taarifa hali ambayo itawezesha kufahamika na kutumika.

“Mmebahatika kuwepo ndani ya mradi huu wa SDGCA, utumieni vizuri katika kuelezea fursa zilizopo kwenye jumuiya hii, ambayo ni muhimu kwa wananchi wa ukanda huu,” alisema.

Akizungumza katika semina hiyo Mwandishi Mwandamizi wa Kituo cha Televisheni cha Channel Ten, Dorcas Raymond, alisema pamoja na dhamira ya waandishi wa habari kutaka kuandika habari za SADC, bado kuna urasimu wa kutoa habari hizo hasa kwa taasisi zenye mamlaka.

Alisema viongozi na watendaji wengi katika taasisi mbalimbali wamekuwa na urasimu wa kuelezea fursa zilizopo katika jumuiya hiyo, hivyo ni vema wakabadilika ili waweze kukidhi hitaji la wawekezaji na wananchi.

Mhariri wa Kituo cha Redio cha Times, Tausi Mbowe alisema bado kuna changamoto ya waandishi wa habari nchini kuandika habari za SADC hali ambayo inasababisha wasiingie kwenye ushindani wa tuzo za uandishi wa habari za jumuiya hiyo.

Mbowe aliitaka SDGCA kuhamasisha matumizi ya kiswahili katika utoaji wa tuzo, ili kuweza kuwavutia waandishi wakitazania kuandika habari za SADC kwa kina.

Msanifu Kurasa wa Gazeti la Mwananchi, Kalunde Jamal, aliwataka waratibu wa mradi kuendelea kutoa mafunzo kwa waandishi wa habari wa Tanzania, ili waweze kuzitambua fursa ambazo zipo na kuzitolea taarifa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

Oryx gesi yagawa mitungi, majiko 100 kwa waandishi wa habari Dar

Spread the loveKAMPUNI ya Oryx Gesi Tanzania imegawa mitungi 100 ya gesi...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mavunde ataja malengo “Vision 2030”

Spread the loveWAZIRI wa Madini amesema dhana ya “Vision 2030” inakusudia kuiendeleza...

Habari MchanganyikoMichezo

Wanamichezo Mei Mosi wachangia wahitaji vitu vya mil. 11.5

Spread the loveWanamichezo wanaoshiriki Michezo ya Mei Mosi Taifa 2024 jijini Arusha...

Habari Mchanganyiko

TMA yapongezwa kuimarisha ubora na usahihi wa taarifa za Hali ya Hewa

Spread the love  WAFANYAKAZI wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA),...

error: Content is protected !!