Friday , 26 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Vyama vya wafanyakazi wakumbushwa kanuni
Habari Mchanganyiko

Vyama vya wafanyakazi wakumbushwa kanuni

Wafanyakazi wa kiwanda cha maziwa cha Azam wakiwa kazini
Spread the love

SERIKALI imewataka watendaji wa vyama vya wafanyakazi kuzisoma, kuzitambua na kuzitumia vyema kanuni na sheria za kazi ili kutatua migogoro ya wafanyakazi na waajiri bila upendeleo na kuleta tija kwa Taifa, anaandika Christina Haule.

Wito huo ulitolewa jana na Kamishna wa kazi, Hilda Kabisa wakati akifungua mkutano wa watendaji wa vyama vya wafanyakazi na waajiri kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Erick Shitindi uliofanyika mkoani Morogoro.

Kabisa amesema kufuatia kuwepo kwa malalamiko ya wafanyakazi ya madai kuwa watendaji wa vyama vya wafanyakazi wanatatua migogoro ya wafanyakazi dhidi ya waajiri kwa kuwapendelea waajiri bila kukumbuka kuwa wanatakiwa kutenda wajibu wao bila upendeleo ni wazi kuwa viongozi hao wamezisahahu kanuni na sheria za kazi ambazo wanapaswa kuzifuatwa ili kuleta amani.

“Kama kutakuwa na upendeleo upande mmoja wakati wa utatuzi wa migogoro ya wafanyakazi, hakutakuwa na amani,” amesema Kabisa.

Amesema watendaji wa vyama vya wafanyakazi wanapaswa kutimiza wajibu wao, kwani wao ni kiungo sahihi kwa wafanyakazi na waajiri ili kukuza uchumi wa nchi.

Naye Katibu Mkuu wa Chama cha Wafanyakazi wa Malori Tanzania, Greyson Unile amesema elimu inapaswa kutolewa kwa wafanyakazi na waajiri ili kuweza kutatua changamoto zinazowakabili wote kwa pamoja na kufanya kushindwa kutekeleza wajibu wao vyema sehemu za kazi.

Unile amesema, zipo changamoto za uelewa wa namna ya kutekeleza masuala ya ajira mahala pa kazi kwa waajiri kufuatia waajiri kutokubali kutekeleza sheria huku wakiwaona watendaji wa vyama vya wafanyakazi kuwa ni adui na sio wazuri kwao.

Amesema, yapo masuala ya kazi ambayo wafanyakazi wanapaswa kuyazingatia ili kuboresha suala la ajira na kwamba wafanyakazi wameonekana kutoyazingatia kutokana na uelewa mdogo.

Hata hivyo Katibu msaidizi wa chama hicho, Yasini Kabingwa ameishauri serikali kuongeza bajeti ya wizara hiyo ili elimu iweze kutolewa na kuimarisha nafasi za watendaji sababu kufuatia maofisa wa kazi kuwa wachache katika mikoa hufanya huduma kushindwa kutolewa vyema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Wakili: Ukimpa zawadi mwenza marufuku kumpora hata mkiachana

Spread the love  WANANDOA na watu waliko kwenye mahusiano ya kimapenzi, wamekumbushwa...

Habari Mchanganyiko

Majaliwa: Mvua zimesababisha vifo vya watu 155, kuendelea hadi Mei

Spread the love  WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amesema mvua kubwa za El-Nino...

Habari Mchanganyiko

Exim Bank yatoa  vitanda kwa shule ya Jeshi la Polisi Moshi

Spread the love  BENKI ya Exim imekabidhii  seti ya vitanda kwa Shule...

Habari Mchanganyiko

NBC yakabidhi vitanda Shule ya Polisi Moshi

Spread the loveBenki ya NBC imekabidhi msaada wa vitanda 28 kwa Shule...

error: Content is protected !!