Sunday , 25 February 2024
Home Habari Mchanganyiko Wauaji wa Kibiti wahofiwa kujificha Dar
Habari Mchanganyiko

Wauaji wa Kibiti wahofiwa kujificha Dar

Simon Sirro, Kamishna wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam
Spread the love

SIMON Sirro, Kamishna wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, amewataka wakazi wa jiji hilo kuwa makini hasa katika kipindi hiki uchunguzi dhidi ya waliotekeleza mauaji ya askari nane, Kibiti, Pwani, anaandika Hamisi Mguta.

Rai hiyo ameitoa leo ofisini kwake kufuatia msako uliodaiwa kuwa mkali kwa majambazi walioshiriki mauaji hayo huku akiwataka madereva bodaboda kuwa makini na abiria wanaowabeba.

“Watu hawa wengi naamini wamekimbilia Dar es Salaam, sina maana ya kuwatia hofu lakini Dar es Salaam na Pwani tunaingiliana sana na mtu akijificha huku inakuwa ni ngumu sana kumpata kama huwezi kuwa na ujanja wa kutosha,” amesema Kamanda Sirro.

Amefafanua kuwa ni vizuri madereva hao wakajenga utaratibu wa kuwa na viongozi ambao watasimamia usalama kwa kuchukua namba ya simu ya abiria na hata wakati mwingine ikiwezekana akapiga picha mtu mnayemtilia mashaka.

“Muda ambao unajua ni mbaya anakuja mteja anataka umpeleke mahala fulani, na unajua ni pori ni lazima ujiulize, maanake wengine kwenye vijiwe unakuta hawapendani na najua kuna watu wanaendesha boda boda kwa ajili ya kufanya uhalifu,” amesema.

Wakati huo huo amewaambia waaandishi wa habari kuwa mnamo Aprili, 15 majira ya 07;00 usiku maeneo ya Kiwalani kwa Ally Mboa, Jeshi hilo limekamata silaha moja aina ya ‘shotgun’ ambayo imekatwa kitako na mtutu na huku namba zake zikiwa zimefutwa.

“Silaha ilipatikana wakati askari wa doria wakiwa katika maeneo hayp ambapo walihisi harufu ya bangi na kuanza kufuatilia ili kubaini ndipo ghafla watu wawili wasiofahamika walikurupuka na kupanda pikipiki (haikusomeka namba) kisha kuangusha begi lenye ambalo lilibainika kuwa na silaha,” amesema.

Aidha katika kuipekua zaidi walikuta risasi nne zikiwa zimefungwa kwenye mfuko wa plastiki pamoja na jaketi jeusi na kofia.

 

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoTangulizi

25 wafariki dunia katika ajali Arusha

Spread the loveWatu 25 wamefariki dunia papo hapo mkoani Arusha katika ajali...

Habari Mchanganyiko

“Jamii ielimishwe faida za uhifadhi”

Spread the loveWIZARA ya Maliasili na Utalii imesema ili kukabiliana na migongano...

Habari Mchanganyiko

Shahidi aeleza Nathwani alivyomshambulia jirani yake

Spread the loveSHAHIDI ambaye ni fundi Seremala, Dominic Mpakani (43) ameileza mahakama...

Habari Mchanganyiko

DCEA, TAKUKURU waunganisha nguvu kupamba na dawa za kulevya, rushwa

Spread the love  MAMLAKA ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya...

error: Content is protected !!