Friday , 3 May 2024
Home Kitengo Biashara Vodacom yazindua kampeni ya ‘Biashara Pamoja, Tuamini Sisi’, katika maonyesho ya Sabasaba
Biashara

Vodacom yazindua kampeni ya ‘Biashara Pamoja, Tuamini Sisi’, katika maonyesho ya Sabasaba

Spread the love

 

KATIKA kutekeleza adhma yake ya kutumia ubunifu wa kidigitali kuongeza ufanisi kwenye shughuli mbali mbali ikiwemo zile za kibiashara, kampuni ya mawasiliano na teknolojia ya Vodacom Tanzania kupitia kitengo cha Vodacom Business imezindua kampeni ya biashara pamoja, tuamini sisi inayolenga kutoa suluhisho za kidigitali kwa biashara ndogo, za kati na makampuni makubwa pamoja na taasisi za kiserikali. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo ulioanyika katika Maonyesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa, maarufu kama Sabasaba yanayoaendelea jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade), Latifa Khamis amepongeza ubunifu unaofanywa na Vodacom kwenye kurahisisha shughuli za kiuchumi za Watanzania.

“Nichukue fursa hii kuipongeza Vodacom kwa huduma zao za kibunifu zilizojikita kwenye ulimwengu wa kidigitali ambao Tanzania na dunia tunaelekea. Leo, wakizundua huduma zao zinazotoa ufumbuzi wa suluhisho mbalimbali kwa wafanyabiashara, wajasiriamali na taasisi za kiserikali, ningependa kuwapongeza kwa kutumia maonyesho ya sabasaba kama jukwaa rasmi la kuzindua kampeni yao maana maonyesho haya yanakutanisha maelfu ya biashara ambazo zitanufaika na huduma kutoka Vodacom Business.

“Kuamua kutuwezesha na huduma ya kuunganishwa na mtandao wa intaneti bila ya malipo kwa mwaka mzima. Ushirikiano huu utatuwezesha TanTrade kurahisisha shughuli zetu za utoaji wa mafunzo na makongamano mbalimbali ambazo zinalenga kuwajengea uwezo wafanyabiashara wadogo na wa kati,” alisema Latifa.

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade), Latifa Khamis

TanTrade ambao ndio waandaaji wa maonyesho ya Biashara ya Kimataifa ya kila mwaka, maarufu kama Sabasaba, mbali na kuandaa tukio hili kubwa kitaifa na kimataifa, hujihusisha na shughuli mbalimbali zinazoratibiwa na Wizara ya Viwanda na Biashara ikiwemo kuwaunganisha wafanyabiashara wa ndani na kimataifa, kutoa fursa kwa wafanyabiashara wa ndani kutangaza biashara zao pamoja na kutoa mafunzo, kuendesha semina na makongamano mbalimbali yanayowakutanisha wadau tofauti wa biashara na uwekezaji nchini.

“Katika ulimwengu wa sasa, hatuwezi kukwepa mapinduzi yaliyoletwa na mapinduzi ya kidigitali nchini. Katika hotuba yake wakati wa uzinduzi wa maonyesho ya Sabasaba jana, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Kassim Majaliwa alidokezea namna nguvu ya kidigitali inavyoweza kutumika kwa manufaa ya wafanyabiashara kwa kuwakutanisha na wateja kutoka sehemu mbalimbali. Ningependa kuwashukuru Vodacom na huduma ya intaneti ya mwaka mmoja bila ya malipo.

“Kama mnavyojua, mojawapo ya majukumu ya TanTrade ni kukuza biashara nchini ambapo ili biashara ziendelee tunatoa mafunzo na kuendesha makongamano mbalimbali kwa wajasiriamali na wafanyabishara ili kuwajengea uwezo, na kuwakutanisha na wadau. Uwepo wa intaneti hii utatuongezea ufanisi na wigo aswa kupitia mafunzo ya mtandaoni hivyo kuwafikia wafanyabiashara wengi zaidi Tanzania,” alimalizia Mkurugenzi Mkuu wa TanTrade.

Naye kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania Plc, Philip Besiimire ameipongeza TanTrade kwa mafanikio yanayoendelea kujidhuhirisha kupitia Maonyesho ya Kimataifa ya Biashara ya Sabasaba ambapo idadi ya washirki makampuni ya ndani na nje ya nchini inazidi kuongezeka kila mwaka.

“TanTrade wanastahili pongezi kwa jitihada zake endelevu katika kuwapatia wafanyabiashara jukwaa la kuonyesha na kutangaza biashara zao kwa Watanzania na wageni mbalimbali wanaotembelea. Kupitia dhamira yake hiyo, nasi Vodacom tumeona ni vyema kuunga mkono shughuli zake kwa kuwasogezea wafanyabiashara huduma thabiti na bora zitakazowaongezea ufanisi katika utendaji wao kama vile malipo ya biashara kupitia M-Pesa, intaneti ya kasi ya 4G na 5G na nyingine nyingi,” alielezea Besiimire.

Kwa upande wake Mkuu wa Masoko na Uwezeshaji kutoka Vodacom Tanzania, Aileen Meena aligusia huduma kemu kemu zinazotolewa na Vodacom Business na kuwahimiza wafanyabiashara walioko saba saba na Tanzania kwa ujumla kuchangamkia fursa hizo.

“Leo, Vodacom inayo furaha kuwatangazia wateja wetu na Watanzania kwa ujumla kuwa tumekuja na huduma kabambe za kidigitali ambazo zitarahisisha uendeshaji na utoaji wa huduma. Hii inajumuisha huduma kama vile intaneti yenye ufanisi na kasi zaidi kwa njia ya 4G na 5G, huduma ya M-Pesa maalum kwa biashara, suluhisho mbalimbali kwa wafanyabiashara kwa njia ya mtandao, vifaa vyenye uwezo wa kufuatilia mwenendo wa shughuli za kibiashara (tracking), kuhifadhi taarifa kwa njia ya mtandao (hosting solutions), M-Kulima kwa ajili ya wakulima na wadau wa sekta kilimo, pamoja na kuwawezesha wafanyabiashara kuwafikia wateja wengi kwa wakati mmoja kupitia jumbe fupi kwa mkupuo.

“Kwa kuongezea, tumerahisisha zoezi la kuwasajili wafanyabiashara wapya kwa njia ya simu ambapo sasa itachukua chini ya dakika 30 tu! Napenda kutoa wito kwa taasisi mbalimbali za kiserikali, wafanyabiashara na sekta binafsi kuitumia vema fursa hii kwa kujiunga nasi ili pamoja tukuze biashara zao,” alimalizia Aileen.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Biashara

Cash Days Promo mamilioni yanakusubiri, cheza kupitia Meridianbet kasino 

Spread the love  JIANDAE kwa mshangao wa kustaajabisha Meridianbet kasino ya mtandaoni...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NBC yazindua huduma maalum kwa wastaafu

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) imezindua huduma maalum kwa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB yazindua akaunti ya Kikundi

Spread the loveBenki ya NMB imezindua akaunti ya kikundi yenye  maboresho makubwa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Wafanyakazi waidai STAMICO mishahara ya bilioni 1

Spread the loveWALIOKUWA wafanyakazi wa mgodi wa Shirika la Madini la Taifa...

error: Content is protected !!