December 7, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Viongozi wa dini wavutana mbele ya Rais Magufuli

Askofu Josephat Gwajima

Spread the love

ASKOFU wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Mchungaji Amani Lyimo amevutana na Askofu Mkuu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima kuhusu usajili wa makanisa hapa nchini. Anaripoti Regina Mkonde … (endelea).

Akizungumza katika Mkutano wa Viongozi wa dini wa madhehebu mbalimbali na Rais John Magufuli, Mchungaji Lyimo amedai kuwa, sasa hivi injili imekuwa biashara na kuitaka serikali kudhibiti usajili wa makanisa kwa kuanzisha kamati maalumu itakayosimamia usajili na maadili ya makanisa hayo.

Mchungaji Lyimo amesema kuwa “Kama mtakumbuka viongozi wa dini kipindi cha uongozi wa Mwalimu Julius Nyerere ilikuwa dini au dhehebu jipya linaanza, kabla ya kusajiliwa, viongozi wa dini wanajadili hilo dhehebu , wanapeleka maoni yao wizara ya mambo ya ndani kisha linasajiliwa, sasa hivi kuna makanisa mengi, injili imekuwa biashara.

Kuwe na kamati maalum ambayo itashughulikia usajili wa viongozi wa dini, hekima za wazee zinaweza kutumika katika kusuajili wakishirikiana na watendaji wao.”

Akijibu kuhusu pendekezo hilo, Askofu Gwajima amesema si sahihi kwa serikali kubana makanisa kwa kuwa uwepo wa madhehebu mengi yanayohubiri injili inavyotakiwa inakuwa Baraka kwa nchi.

“Pastor Lyimo amemaliza kuzungumza nikaona akasema ni muhimu serikali ifanye utaratibu kuwa mgumu, nina fikiri jambo hilo si sahihi, sababu ziko nyingi sana, ukienda kila mahali hatua moja utakuta baa hatua moja grosari, sehemu nyingine haina baa watu wanakunywa pombe.

Madhehbu yanayohubiri sawa sawa injili yanapokuwa mengi inakuwa Baraka kwa nchi, nimshauri kwamba madhehebu yasipunguwe isipokuwa yaongezeke na kuhubiri yanayotakiwa kuhubiriwa,” amesema Askofu Gwajima.

error: Content is protected !!