Saturday , 27 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Viongozi 140 waiandikia barua WHO kutaka dawa ya corona iwe bure 
Habari Mchanganyiko

Viongozi 140 waiandikia barua WHO kutaka dawa ya corona iwe bure 

Cyril Ramaphosa, Rais wa Afrika Kusini
Spread the love

RAIS wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa na Imran Khan, Waziri Mkuu ni miongoni mwa viongozi 140 waliosaini barua kwenda Shirika la Afya Duniani (WHO), wakishauri dawa ya corona itakapopatikana, igawiwe bure kwa watu wote. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa…(endelea).

Wamesema, dawa pamoja na chanjo yake inapaswa kugawiwa bure, na iwe haki ya kila mwanadamu kupata dawa hiyo ili aishi.

“Dawa ya corona haipaswi kuwa biashara duniani, wanasayansi watakaovumbua wawaeleze wanasayansi wenzao namna ya utengeneza.”

“Serikali za mataifa lazima ziungane duniani kote ili kuhakikisha kwamba, pale dawa itapopatikana, inazalishwa kwa wingi na haraka na zinasambazwa kwa watu wote, katika mataifa yote bila malipo,” barua hiyo imeeleza, na kuongeza:

“Tiba, utambuzi na uvumbuzi wowote ulio na uhusiano na CIVID-19, unapaswa kuelezwa kwa mataifa yote bila ubaguzi.”

Pia, Rais Ramaphosa jana jioni Jumatano tarehe 13 Mei 2020, alipohutubia taifa hilo alisema, nchi yake licha ya maambukizi kufika 12,000, bado mpango wa kuondoa vikwazo vya kukaa ndani unaendelea na anatarajia mwishoni mwa mwezi huu, watu wataendelea na shughuli zao kama kawaida.

Ramaphosa alisema, “baadhi ya maeneo yaliyoathiriwa zaidi na COVID-19 nchini humo yataendelea na utaratibu wa kujifungia mpaka maambukizi yatakapopungua.”

Mpaka tarehe ya leo, Afrika Kusini imeshuhudia vifo 219 vilivyotokana na ugonjwa wa corona.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Wakili: Ukimpa zawadi mwenza marufuku kumpora hata mkiachana

Spread the love  WANANDOA na watu waliko kwenye mahusiano ya kimapenzi, wamekumbushwa...

Habari Mchanganyiko

Majaliwa: Mvua zimesababisha vifo vya watu 155, kuendelea hadi Mei

Spread the love  WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amesema mvua kubwa za El-Nino...

Habari Mchanganyiko

Exim Bank yatoa  vitanda kwa shule ya Jeshi la Polisi Moshi

Spread the love  BENKI ya Exim imekabidhii  seti ya vitanda kwa Shule...

Habari Mchanganyiko

NBC yakabidhi vitanda Shule ya Polisi Moshi

Spread the loveBenki ya NBC imekabidhi msaada wa vitanda 28 kwa Shule...

error: Content is protected !!