November 29, 2022

Uhuru hauna Mipaka

TFF yafafanua juu ya matumizi ya fedha za FIFA

Ofisi za TFF

Spread the love

KATIBU Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania ( TFF), Wilfred Kidao ametoa ufafanuzi juu ya matumizi ya fedha kutoka Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani (FIFA), Shilingi 2.3 bilioni ambazo hupewa kila mwaka kama mwanachama kwenye shirikisho hilo baada ya kutokea kwa sintofahamu. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea).

Hivi karibuni kumeibuka mijadala kwa wadau wa soka nchini kuuliza namna matumizi ya fedha kutoka FIFA zinazotumika ndani ya shirikisho hilo kiasi cha kupelekea katibu mkuu wa TFF kutoa ufafanuzi huu.

Katika maelezo yake Kidao amesema kuwa fedha hizo ambazo zinatolewa kwa awamu mbili kwa mwaka mwezi Januari na Juni zikiwa zimeainishwa kwa ajili ya uendeshaji wa shughuli za uendeshaji Taasisi katika kipindi cha mwaka mzima.

“Kwa kila mwaka FIFA wanatupa Tanzania Shilingi 2.3 bilioni kwa ajili ya kusaidia uendeshaji wa taasisi katika shughuli zake za kila siku kwa mwaka mzima kama mishahara ya makocha timu ya Taifa na wafanyakazi wa shirikisho, programu za vijana na timu za wanawake, mitandao ya kijamii ya TFF na shughuli nyingine za taasisi,” alisema Kidao

Katibu huyo aliongezea kuwa katika awamu ya pili ya fedha hizo ambazo zinatoka mwezi Julai, FIFA hutoa masharti kumi ambayo kama mwanachama lazima uwe umevitimiza katika mwaka huo husika.

“Cha kwanza wanataka timu yako ya taifa (Senior A Team) kwa upande wa wanaume na wanawake lazima ziwe zimecheza mechi za kimataifa zisizopungua nne, kigezo kingine ni kuwa na timu za taifa za vijana mbili ambazo lazima ziwe zimecheza mechi nne kila moja vilevile unatakiwa uwe na timu za wanawake sambamba na Ligi ya vijana isiyopungua timu 10 sambamba na programu za waamuzi,” amesema Kidao.

Kidao aliongezea kuwa fedha zote zinazotoka kwenye shirikisho hilo lazima zifanyie ukaguzi (Fifa centre review) ambao wanafanya wenyewe kwa kushirikiana na makampuni makubwa kutoa nje ya nchi.

Katika hatua nyingine Kidao ameeleza kurejea kwa michezo ya Ligi Kuu Tazania Bara na kusema kuwa jambo hilo kwa sasa linasubili uamuzi wa serikali kutokana na mwenendo wa janga la Corona.

error: Content is protected !!