Monday , 27 May 2024
Home Kitengo Michezo Vigogo 14 kuiongezea nguvu Taifa Stars kufuzu AFCON
Michezo

Vigogo 14 kuiongezea nguvu Taifa Stars kufuzu AFCON

Spread the love

SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) leo limetangaza kamati ya watu 14 yenye lengo la kuisaidia timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ kufuzu Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) zitakazofanyika Misri mwaka huu. Anaripoti Kelvin Mwaipungu … (endelea).

Kamati hiyo itaongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ambaye Mwenyekiti, huku katibu wake atakuwa Mhandisi ni Mhandisi Hersi Said.

Wajumbe wa kamati hiyo ni Mohamed Dewji, Haji Manara, Jerry Muro, Farouk Barhoza, Salim Abdallah, Mohamed Nassor, Patrick Kahemele, Abdallah Bin Kleb, Tedy Mapunda, Philimon Ntaihaja, Farid Nahid na Faraji Asas.

Jukumu kubwa la kamati hiyo itakuwa ni kuhakikisha timu hiyo inapata ushindi kwenye mchezo wake wa mwisho wa kundi L dhidi ya Uganda utakaochezwa mwezi Machi mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Kwa sasa Stars ina pointi tano na kushika nafasi ya pili kwenye msimamo wa kundi hilo mara baada ya kucheza michezo mitano ikiwa sawa na Lesotho nao wenye pointi kama hizo wakitofautiana mabao ya kufungwa na kushinda.

Ni miaka 39 imepita tangu mara ya mwisho timu ya Taifa ya Tanzani kufuzu katika michuano ya kombe la mataifa huru ya Afrika, wakati huo kikosi cha Stars kilikuwa na nyota kama Athumani Mambosasa, Juma Pondamali, Taso Mutebezi, Jelah Mtagwa, Leodgar Tenga

Mohamed Kajole, Husein Ngulungu, Mtemi Ramadhan, Juma Mkambi, Omari Hussein, Mohamed Masewa, Thuweni Ally, Peter Tino, Ahmed Thabit, Charles Boniface, Salim Amiri, Adolf Richard, Zamoyoni Mogela, Martin Kikwa na George Kulagwa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoMichezo

NBC yakabidhi Kombe la Ubingwa wa Vijana (U20) kwa Kagera Sugar FC

Spread the loveMdhamini mkuu wa Ligi ya Vijana chini ya miaka 20...

Michezo

NBC yakabidhi Kombe la Ubingwa wa  Ligi Kuu ya NBC, yaahidi maboresha zaidi

Spread the loveMdhamini mkuu wa Ligi Kuu ya NBC (NBC Premiere League),...

Michezo

Unamalizaje Jumapili hujabeti na Meridianbet?

Spread the love JUMAPILI ya leo tutashuhudia mitanange kibao ambayo itamalizika kuanzia...

Michezo

Jipigie pesa na Meridianbet leo hii

Spread the love KAMPUNI kubwa ya ubashiri Tanzania inakwambia hivi huu ndio...

error: Content is protected !!