October 2, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Chadema, serikali wavutana kuhusu Lissu

Tundu Lissu, Makamu Mwenyekiti wa Chadema

Spread the love

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimeeleza kutishika na matamshi wanayodai kutolewa na mmoja wa mawaziri katika Serikali ya Awamu ya Tano na kwamba, yanatishia usalama wa Tundu Lissu. Anaripoti Faki Sosi… (endelea).

Akizungumza na waandishi wa habari leo tarehe 20 Februari 2019 Patrick Ole Sosopi, Mwenyekiti wa Baraza Vijana la Chadema (Bavicha) amesema, matamshi hayo yanazidisha mashaka kuhusu shambulio la Lissu ambaye ni Mbunge wa Singida Mashariki.

Sosipi amedai kuwa, kauli ya kutaka kumzamisha Lissu kama mtumbwi baada ya kuponea chupuchupu na kuanza kufanya ziara Ulaya na Marekani huku akiendelea na matibabu nchini Ubelgiji, inaleta taswira hasi.

Lissu ambaye pia ni Mnadhimu Mkuu wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni alishambuliwa tarehe 7 Septemba 2017 eneo la Area ‘D’ Dodoma.

 Tazama hapa video yote……

error: Content is protected !!