Friday , 19 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Prof. Lipumba aanza kupotea
Habari za SiasaTangulizi

Prof. Lipumba aanza kupotea

Maalim Seif Sharrif Hamad
Spread the love

KATIBU Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Shariff Hamad, amemzidi kete, Prof. Ibrahim Lipumba, mwenyekiti wa chama hicho anayetambuliwa na Msajili wa Vyama vya Siasa, Francies Mutungi. Anaripoti Regina Mkonde … (endelea).

Chama cha CUF, kimekumbwa na mgogoro mkubwa wa uongozi kwa takribani miaka mitatu sasa, kufuatia Jaji Mutungi kuamua kumrejesha kwenye uongozi, kinyume cha sheria za vyama vya siasa, kanuni na taratibu, Prof. Lipumba, ambaye alijiuzulu wadhifa huo, kipindi cha kuelekea uchaguzi mkuu wa 2015.

Akizungumza na MwanaHALISI ONLINE, Naibu Mkurugenzi wa Habari na Mawasiliano na Umma, Mbarala Maharagande amesema, uongozi wa chama hicho uliyopo chini ya katibu wake mkuu, Maalim Seif Shariff Hamad, itawasilisha orodha mpya ya wajumbe wa Bodi ya wadhamini.

Kwa mujibu wa Magaragande, orodha hiyo imepelekwa leo tarahe 20 Februari, kwa Wakala wa Serikali wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA).

Maamuzi hayo yamefikiwa na Baraza Kuu la uongozi la chama hicho (BKT), lililokutana jana tarehe 19 Februari 2019, jijini Dar es Salaam.

 “Tayari tumepeleka orodha mpya kwa RITHA ili kutekeleza maamuzi ya baraza kuu lililokutana jana (Jumanne), jijini Dar es Salaam. Tumefanya haya ili kukidhi matakwa ya sheria,” ameeleza.

Amesema, “uteuzi huu wa sasa, umefanyika baada ya Mahakama Kuu, Kanda ya Dar es Salaam, kuifuta bodi ya Prof. Lipumba kwa maelezo kuwa haipo kwa mujibu wa sheria na kuikosoa bodi ambayo iliundwa na kambi ya Maalim.”

Madai kuwa Prof. Lipumba ameanza kuingia mitini zinathibitishwa na hatua ya mkurugenzi wake wa Habari na Mawasiliano, Abdul Kambaya, kushindwa kuongea na waandishi wa habari, kujibu swali juu ya hatma yao ndani ya chama hicho.

Kambaya, tofauti na ilivyokuwa siku za nyuma, alisema, “sina la kusema. Swali kwamba Maalim Seif amepeleka orodha mpya ya wajumbe wa Bodi na matokeo yake, waulizeni wahusika wenyewe. Mimi siko upande huo.”

Kambaya amesema, “endeleeni kuandika mnavyotaka.” Kabla ya mwandishi kuendelea kuuuliza swali jingine, haraka Kambaya akakata simu. Mwandishi alipigia tena na tena simu hiyo, lakini haikupokelewa.

Wachambuzi wa mambo ya kisiasa wanasema, ikiwa Maalim Seif atafanikiwa kusajili m “Bodi yake ya Wadhamini,” atakuwa – yeye na wenzake waliowengi – ndio wamiliki halali wa fedha na mali za chama hicho.

Kesi ya kupinga bodi ya Prof. Lipumba, ilifunguliwa mahakamani na Mbunge wa Malindi, Unguja, Ally Saleh. Kesi hiyo iliyopewa Na. 13 ya mwaka 2017, pamoja na mengine, ilikuwa inapinga uundwaji wa bodi ya Prof. Lipumba kwa maelezo kuwa ni kinyume na Katiba ya chama hicho.

Katika mashitaka yake mahakamani, mbunge huyo aliiomba mahakama itamke kuwa ni ipi bodi halali kwa mujibu wa sheria za nchi na Katiba ya CUF 1992 toleo la mwaka 2014. Kesi ilisikilizwa na kufanyiwa maamuzi na Jaji Benhajji Masoud.

Katika hatua nyingine, Maharagande amesema, baraza kuu la chama hicho, limemuelekeza Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), kufanya uchunguzi maalum wa fedha za ruzuku zilizotolewa na msajili wa vyama kwa Prof. Lipumba.

Amesema, “uchunguzi huo unalenga kujiridhisha matumizi ya fedha hizo, kwa kuwa zilikabidhiwa kwa mtu asiye sahihi.”

“Msajili wa vyama alitoa fedha za umma pasipo idhini ya bodi halali ya CUF. Kwa makusudi kabisa, Jaji Mutungi aliamua kuzipeleka fedha hizo kwenye akaunti ambayo haikuwa halali, ili kumsaidia Prof. Lipumba kutimiza malengo yake,” ameeleza.

Amesema, “Wabunge wetu watafanya hivyo hivi karibuni, wanajiandaa kupeleka taarifa rasmi ya kuomba ukaguzi huo maalum ufanyike.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

KimataifaTangulizi

Mkuu wa majeshi Kenya afariki, Ruto atangaza maombolezo

Spread the loveRais wa Kenya, William Ruto ametangaza maombezo ya siku tatu...

Habari za SiasaTangulizi

Tanzania, Uturuki zanuia kukuza biashara, uwekezaji

Spread the loveSERIKALI za Tanzania na Uturuki zimekubaliana kuendeleza dhamira ya kuimarisha...

Habari za Siasa

Tume huru ya uchaguzi yatangaza ajira watendaji daftari wapiga kura

Spread the love  TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), imetangaza nafasi...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema yatangaza ruti awamu ya pili maandamano

Spread the love  CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimesema awamu ya...

error: Content is protected !!