October 2, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Utata wa mali za Mugabe waibuka

Marehemu Robert Mugabe enzi za uhai wake

Spread the love

TERRENCE Hussein, Mwanasheria wa Familia ya aliyekuwa Rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe, amewataka waliomtuhumu kiongozi huyo kujilimbikizia mali nje ya nchi, kupeleka taarifa ya mali zake mahakamani,  ili zisajiliwe. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa…(endelea).

Kauli ya mwanasheria huyo imetokana na tuhuma kutoka kwa baadhi ya watu na nchi zilizokuwa zinakosoa utawala wa Mugabe, ya kwamba kiongozi huyo alikuwa anajilimbikizia mali nje ya nchi.

Kufuatia tuhuma hizo, leo tarehe 5 Desemba 2019 Hussein ameeleza kuwa, nchi zilizokuwa zinamtuhumu Mugabe zinatakiwa kuthibitisha, kwamba alikuwa na mali nje ya nchi.

Ili mali zake zisajiliwe mahakamani, kwa ajili ya kugawiwa kwa warithi wake.

“Hili ndio jambo zuri unaposema uongo, uongo wote utafunuliwa. Mali ziko wapi? amehoji Hussein.

Hatua hiyo imekuja baada ya Mahakama Kuu ya mjini Harare  kumteua Bona Chikore, binti wa marehemu Mugabe, kutambua mali alizoacha baba yake, ili zigawanywe kwa warithi wake.

Hussein ameeleza kuwa, Familia ya Mugabe imebariki Bona kuwa msimamizi wa mirathi.

Hivi karibuni Serikali ya Zimbabwe kupitia gazeti lake la The Herald,  lilitangaza mali zilizoachwa na Mugabe, ikiwemo fedha zaidi ya Sh. 22 bilioni, nyumba nne zilizoko mjini Harare, magari 10 na mashamba.

Hata hivyo, kabla Mugabe kufariki, alikuwa anatuhumiwa kujilimbikizia mali ikiwemo fedha na nyumba,kwenye nchi za Asia hasa Hong Kong, ambako alikuwa anapenda kwenda mapumziko na familia yake.

error: Content is protected !!