Saturday , 4 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Ujenzi daraja la Magufuli wafikia asilimia 78
Habari Mchanganyiko

Ujenzi daraja la Magufuli wafikia asilimia 78

Spread the love

WAZIRI wa Ujenzi, Innocent Bashungwa amesema ujenzi wa daraja la John Pombe Magufuli (Kigongo – Busisi) lenye urefu wa kilomita tatu na Barabara unganishi zenye jumla ya kilometa 1.66 jijini Mwanza, umefikia asilimia 78. Anaripoti Danson Kaijage, Mwanza … (ndelea).

Daraja la Magufuli likiendelea kujengwa

Ameyasema hayo jana tarehe 11 Oktoba 2023 jioni akiwa Mwanza katika ziara ya kukagua Daraja hilo linalounganisha Barabara Kuu ya Usagara – Sengerema – Geita katika Ziwa Victoria kwa kugharimiwa na Serikali kwa jumla ya Sh 716.3 bilioni.

Amesema Rais Samia Suluhu Hassan ameupa kipaumbele ujenzi wa daraja hilo kwa kuhakikisha mkandarasi hatoki nje ya mradi kwa kutoa fedha  kuwezesha madai yote kulipwa ndani ya muda ili kuhakikisha anafanya kazi bila kusimama.

Aidha, Bashungwa amemuomba Mkuu wa Mkua wa Mwanza, Amos Makalla kupita mara kwa mara katika mradi huo ili kuhakikisha kazi inaendelea kwa sababu mkandarasi hana sababu yeyote ya kutoendelea na kazi kwani malipo yote yanafanyika kwa wakati.

“Tunaposema Kazi Iendelee ni kama hivi miradi yote inayotumia mabilioni ya fedha inatekelezwa hivyo nawaomba watanzania tuendelee kuwa wamoja kwani mradi huu utafungua fursa za kiuchumi kwa wananchi wa kanda ya ziwa na mikoa ya jirani” ameongeza Bashungwa.

Awali akitoa taarifa ya daraja hilo, Mkurugenzi wa Miradi kutoka Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS), Eng Boniface Mkumbo amesema kuwa hadi sasa mkandarasi ameshalipwa jumla ya Sh 396.3 bilioni ambazo zinajumuisha malipo ya awali pamoja na hati zote za madai 17 alizowasilisha hivyo hadai malipo yoyote.

Amesema kuwa lengo la ujenzi wa daraja hilo ni kuunganisha barabara kuu ya Usagara – Kisesa – Geita yenye urefu wa kilomita 90 katika ushoroba wa ziwa Victoria ambayo inaanzia Sirari mpakani mwa Tanzania na Kenya hadi Mutukula mpakani mwa Tanzania na Uganda (km 774)

Mkumbo amesema kuwa kwa sasa barabara hii inaunganishwa kwa kutumia vivuko vikubwa vitatu na kutokana na idadi kubwa ya magari yanayopita kwa siku huweza kutumia saa mbili hadi tatu kuvusha magari kutoka upande mmoja hadi mwingine.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

RPC Dodoma akabidhiwa bunduki mbili za wahalifu

Spread the love  Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa ya Kulevya...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NBC yazindua huduma maalum kwa wastaafu

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) imezindua huduma maalum kwa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB yazindua akaunti ya Kikundi

Spread the loveBenki ya NMB imezindua akaunti ya kikundi yenye  maboresho makubwa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Wafanyakazi waidai STAMICO mishahara ya bilioni 1

Spread the loveWALIOKUWA wafanyakazi wa mgodi wa Shirika la Madini la Taifa...

error: Content is protected !!