Sunday , 12 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Ugonjwa mpya wa zinaa waibuka Kenya
Habari Mchanganyiko

Ugonjwa mpya wa zinaa waibuka Kenya

Spread the love

WAKATI wanasayansi wakihaha kutafuta dawa ya kutibu Virusi Vya Ukimwi (VVU), nchini Kenya imebainika kuwa kuna ugonjwa mpya unaohusiana na magonjwa ya zinaa. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa…(endelea).

Magonjwa hayo yana uhusiano wa karibu na kisonono (gonorrhea) na wataalamu wa Taasisi ya Utafiti wa Matibabu nchini (KEMRI) wanasema kuwa hayajawahi kuonekana humu nchini awali.

Kutokana na hali huyo wataalam hao wa afya wamewataka Wakenya kuwa waangalifu baada ya kugunduliwa kwa aina mpya ya magonjwa ya zinaa nchini humo.

Naibu mtafiti mkuu katika Kituo cha Utafiti kuhusu Viini katika KEMRI, Profesa Samson Muuo, alisema amegundua kuwa wanawake 424 Wakenya wenye umri wa kuanzia miaka 15 kwenda juu walioshiriki utafiti huo uliofanywa katika hospitali mbili walionyesha dalili za maradhi ya kisonono na chlamydia.

Alieleza vyombo vya habari nchini humo kuwa wahusika walilalamika kuhusu kuwashwa, uchungu na kuvimba kwenye sehemu nyeti, harufu mbaya, kutoka uchafu, kuwashwa wakati wa haja ndogo, kuvuja damu kwa njia isiyo ya kawaida na uchungu kwenye sehemu ya chini ya mgongo.

“Habari hizi zilikusanywa kutoka kwa wanajamii katika sehemu moja na bado zinachunguzwa hivyo basi tutajua hivi karibuni ni wangapi walitumia kinga, historia yao ya kutumia dawa za kuua viini kwa sababu wengi wao waliashiria kuwa wamezitumia hapo awali, maambukizi mengineyo na iwapo wamewahi kupata maradhi kama hayo hapo awali.

“Hatukufanya vipimo vya HIV kwa sababu havikuwa sehemu ya lengo la utafiti.”

Watafitiwa walikuwa wanawake wanaoshiriki ngono na waliofikisha umri wa uzazi zaidi ya miaka 15 na pia walikubali kushiriki utafiti kwa hiari.

“Aina mbili ya jeni tulizogundua kwa jina MtrR na 23S rRNA zinazohusishwa na hali ya kukataa tiba, hazina uhusiano na aina ya maradhi yaliyoripotiwa awali.

“Busia ambao ni mji wa mpakani unatoa mwelekeo bora kuhusu kusambaa kwa ugonjwa huo. Inaweza ikachukuliwa kuwa maambukizi haya yatasambaa kati ya maeneo haya mawili,” alisema Profesa Muuo.

“Katika utafiti huu, chembechembe zilitwaliwa kutoka sehemu nyeti za wanawake walioonesha dalili za maradhi hayo ya zinaa. Aina tatu ya maradhi ya zinaa ikiwemo aina mpya ya kisonono, Chlamydia na Mycoplasma ziligunduliwa katika wanawake hao wote 424 walioteuliwa kushiriki utafiti huo.”

Aidha, Mtaalam wa maambukizi katika Ofisi ya Kimaeneo katika Shirika la Afya Duniani (WHO-AFRO) Shillah Simiyu, alisema Busia ina idadi kubwa ya maradhi ya zinaa kutokana na kiwango cha juu cha shughuli za ngono kutokana na kwamba ni mji wa mpakani ambapo madereva hupumzika wanapokuwa safarini.

1 Comment

  • (i) Ubaguzi wa rangi na ubaguzi dhidi ya watoto kwa misingi ya makabila, lugha na dini umeenea duniani na kuleta athari kwenye mfumo wa haki, usawa na hata KUJISOMEA, limesema Shirika la UN la UNICEF.
    (ii) South Sudan’s refugee crisis remains the largest in Africa. Those displaced within and from South Sudan jointly call for an end to the /conflict for a chance to return to a peaceful home.
    (iii) UNHCR’s support for ~1 million Rohingya refugees in Bangladesh is underfunded. Critical services such as health, housing, water, sanitation and hygiene are at risk.
    (iv) On average, over 40 million people have been estimated to be food insecure every year by the SADC Regional Vulnerability Assessment Programme over the past five years.
    (v) Balaaa NA NI HATARI: Wagandana wakifanya mapenzi, aliewanasisha aeleza alivyofanya, mganga atoa masharti mazito.
    (vi) Wamiliki wa ardhi katika kata ya Mabwepande Wilaya ya Kindondoni jijini Dar es Salaam wameililia serikali wakitaka kuondolewa kwa wavamizi wa ardhi eneo hilo wanaodaiwa kuhatarisha usalama.
    (vii) Americans watched in horror as the terrorist attacks of Sept. 11, 2001, left nearly 3,000 people dead in New York City, Washington, D.C., and Shanksville, Pennsylvania.
    (viii) Mwalimu alikuwa anafundisha shule ya vichaa na alijiwekea utaratibu kuwa kila mwisho wa mwaka atawapa jaribio nani amejaribu kupona ukichaa siku moja alipokuwa darasani alichora mlango ubaoni.
    (ix) Utafiti mkubwa uliofanywa duniani na kuchapishwa katika jarida la lancet umethibitisha kwamba utafiti uliofanywa awali na kuonyesha kwamba hakuna usalama katika unywaji wa pombe.
    (x) Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema mauaji ya kimbari ya Rwanda dhidi ya Watutsi ya mwaka 1994 hayakuwa ya bahati mbaya wala yasiyoweza kuepukika.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Dk. Biteko: Serikali itaendelea kushirikiana na Red Cross

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

Habari MchanganyikoHabari za SiasaTangulizi

Dk.Mpango aagiza trafki kuvaa makoti ya kamera kudhibiti rushwa

Spread the loveMakamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk....

BiasharaHabari Mchanganyiko

PPAA yajipanga kuwanoa wazabuni namna kuwasilisha rufaa kieletroniki

Spread the loveIli kukabiliana na mageuzi yaliyofanyika katika Sheria mpya ya Ununuzi...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Vijana UVCCM Kagera wataka mwenyekiti wao ajiuzulu

Spread the loveVIJANA wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Kagera wamemtaka Mwenyekiti...

error: Content is protected !!