Thursday , 2 February 2023
Home Kitengo Michezo UEFA yapamba moto, Salah usipime
Michezo

UEFA yapamba moto, Salah usipime

Mohammed Salah
Spread the love

 

MSHAMBULIAJI wa Liverpool ambaye pia ni raia wa Misri, Mohamed Salah amezidi kupamba moto kila panapokucha baada ya jana tarehe 19 Oktoba, 2021 kufunga bao mbili na kuisaidia timu yake kuibuka na ushindi ugenini wa mabao 3 – 2 dhidi ya Atletico Madrid katika dimba la Wanda Metropolitania. Anaripoti Damas Ndelema, TUDARCo … (endelea).

Mshambuliaji huyo amekua na kiwango bora tangu mwanzo wa msimu huu kwa kuanzia kwenye Ligi Kuu ya England hadi kwenye michuano ya Klabu Bigwa Barani Ulaya (Uefa Champion League) kwa kufunga magoli muhimu na kuisaidia timu kuchukua pointi tatu muhimu

Katika mechi hiyo ya jana iliyokua ya kuvutia huku timu zikishambuliana kwa zamu, Liverpool walikua wa kwanza kupata magoli yake mawili kupitia kwa Mohamed Salah katika dakika nane na Nabi Keita dakika 13 kabla ya Atletico kuamka na kusawazisha goli zote mbili kupitia kwa mshambuliaji wake Atonie Griezman.

Griezman alitupia mabado hayo katika dakika 20 na dakika 34 lakini katika dakia mya 52 alipata kadi nyekundu kuwafanya Atletico wacheze pungufu.

Pigo hilo liliwapa Liverpool nguvu na kufanikiwa kutawala mchezo huo hadi kusikia dakika ya 78 ambapo Salah aliwapatia bao la tatu na la ushindi kwa njia ya mkwaju wa penalti baada ya Diogo Jota kufanyiwa madhambi kwenye 18.

Hadi kipenga cha mwisho kinapulizwa Liverpool walikua mbele kwa bao 3-2.

Aidha, michuano hiyo ya Uefa iliendelea kwa mechi mbalimbali ambapo mshambuliaji wa PSG raia wa Argentina, Lionel Messi aliisaidia timu yake ya kuibuka na ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Rb leipzig huku goli lingine la PSG likifugwa na Killyne Mbappe ambaye pia alikosa penalti katika mchezo huo

Matokeo mengine ya michuano hiyo ni kama ifuatavyo Club Brugge 1 Vs 5 Manchester City, Porto 1 vs 0 Ac Millan, Sharkta Donestk 0 vs 5 Real Madrid, Inter Milan 3 vs 1 sheriff Fc, Ajax 4 vs 0 Dortimund, Besiktas 1 vs 4 Sporting Cp

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

GGML: Uwanja mpya wa Geita Gold FC kukamilika Mei, 2023

Spread the loveUWANJA wa Magogo unaojengwa na Halmashauri ya Mji wa Geita...

Michezo

Wanafunzi chuo Mwalimu Nyerere wapongezwa kwa ushindi

Spread the love  UONGOZI wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere (MNMA)...

Michezo

Arsenal waipopoa Manchester United

Spread the loveKLABU ya Arsenal inayoshiriki Ligi Kuu England imewatandika Mashetani Wekundu...

Michezo

Mchezaji Singida apoteza maisha mazoezini

Spread the love  MCHEZAJI na kapteni wa timu ya vijana ya Singida...

error: Content is protected !!