Tuesday , 19 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Kesi Mbowe, wenzake: Mahakama yapangua pingamizi yao
Habari za SiasaTangulizi

Kesi Mbowe, wenzake: Mahakama yapangua pingamizi yao

Spread the love

 

MAHAKAMA KUU, Divisheni ya Rushwa na Uhujumu Uchumi, nchini Tanzania imeyatupa mapingamizi mawili ya upande wa utetezi katika kesi inayomkabili kiongozi wa chama kikuu cha upinzani nchini humo cha Chadema, Freeman Mbowe na wenzake watatu. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Mapingamizi hayo yalihusu maelezo ya onyo ya mshtakiwa wa pili katika kesi hiyo ya uhujumu uchumi yenye mashtaka ya kupanga njama za ugaidi ya Adam Kasekwa, yasitumike mahakamani hapo kama sehemu ya ushahidi wa jamhuri na maelezo hayo yalitolewa baada ya Kasekwa kuteswa.

Uamuzi huo wa kesi ndogo ndani ya kesi kubwa, yametolewa leo Jumatano, tarehe 20 Oktoba 2021 na Jaji Kiongozi Mistapha Siyani.

Mbali na Mbowe na Kasekwa, watuhumiwa wengine katika kesi ya msingi ya uhujumi uchumi yenye mashtaka ya kula njama za kufanya vitendo vya ugaidi ni, Halfan Hassan Bwire na Mohammed Abdillah Ling’wenya.

Kesi hiyo ndogo ndani ya kesi ya msingi, imetokana na mapingamizi ya upande wa utetezi, dhidi ya maelezo ya onyo ya mshtakiwa wa pili, Kasekwa, yaliyowasilishwa mahakamani hapo na upande wa jamhuri kama sehemu ya ushahidi wake.

Wakitaka yasitumike kwa madai kuwa yalichukuliwa kinyume cha sheria, ikiwemo mtuhumiwa kuchukuliwa maelezo hayo nje ya muda na bila ya ridhaa yake.

Kasekwa na Ling’wenya walikamatwa tarehe 5 Agosti 2020 maeneo ya Rau Madukani, Moshi Kilimanjaro na kuhojiwa tarehe 7 Agosti mwaka jana, Kituo Kikuu cha Polisi Dar ea Salaam.

Akitoa uamuzi katika pingamizi la muda, Jaji Kiongozi Siyani amesena, kifungu cha sheria namba 50 (2) na cha 51 cha Sheya Mwenendo wa Makosa ya Jinai iliyonyiwa marekebisho 2019, kinaruhusu muda wa kumhoji mtuhumiwa kuongezwa kwa masharti maalum ikiwemo mkuu wa upelelezi kuongeza muda au kuomba kibali cha kuongeza muda huo mahakamani.

Jaji Kiongozi Siyani amesema hoja ya jamhuri kuchelewa kumhoji Kasekwa kwa sababu ya mtuhumiwa huyo kuwasaidia kumtafura mwenzao Moses Lijenge mkoani Kilimanjaro na Arusha, na kumsafirisha kutoka Moshi kuja Dar es Salaam ina mantiki.

“Ni maoni yangu kwamba kuchelewa kwa kuhojiwa au kuchukuliwa maelezo Kasekwa kulikuwa na sababu na kwamba zinafananana matakwa ya sheria ya mwenendo wa makosa ya jinai ya 2019 kifungu cha 50 (2). Matakwa ya sheria hiyo muda uliotumika kumkamata na kumsafirisha kuja Dar haupaswi kuwa ndani ya saa nne ambayo yanapaswa kuhesabiwa,” amesema.

Kuhusu pingamizi la mtuhuniwa kuchukuliwa maelezo kwa vitisho, Jaji Kiongozi Siyani ushahidi wa utetezi haukuthibitisha madai hayo kwa kuwa haukupinga kitabu cha mahabusu (dentetion rejesta) iliyoletwa na jamhuri kama sehemu ya ushahidi wake, kilichoonesha kuwa mtuhumiwa alihojiwa kituo kikuu central Dar.

Awali, mtuhumiwa alidai alichukuliwa maelezo hayo kwa kushinikizwa kituo cha polisi mbweni Dar es Salaam.

Jaji Kiongozi Siyani amesema hakuna mahali mtuhumiwa alipinga kuhojiwa kituo cha polisi Dar, bali alisema alitoa maelezo kwa mateso hivyo mapingamzii ya utetezi ya kwamba hayana mashiko.

“Mapingamizi yamekosa mashiko ya kisheria. Ushahidi kuhusu kupinga kitabu cha mahabusu kilicholetwa mahakamani na jamhuri ambacho kinaonesha kuingia mtuhumiwa ama mahabusu na kutolewa kwa ajili ya kuhojiwa. Na kwamba maelezo yalitolewa kwa rudhaa yake na hilo ndilo hitimisho langu.”

Miongoni mwa mawakili wanaomuwakilisha Mbowe na wenzake katika kesi ya msingi ni, Peter Kibatala, John Mallya, Jeremiah Mtobesya, Fredy Kiwhelu, Dickson Matata, Alex Masaba na Nashon Nkungu.

Wakati wa jamhuri wakiwa ni pamoja naMawakili wa Serikali Waandamizi, Robert Kidando, Abdallah Chavula, Pius Hilla, Nassoro Katuga, Jenetreza Kitali, Tulumanywa Majigo na Ester Martin.

Kufuatia uamuzi huo, kesi ya msingi inaendelea kusikilizwa kwa upande wa jamhuri kuleta ushahidi wake.

Katika kesi hiyo ndogo, mashahidi wa utetezi walikuwa washtakiwa wawili kati ya wanne, Kasekwa na Ling’wenya, ambao walikamatwa pamoja tarehe 5 Agosti 2020, mkoani Kilimanjaro. Pamoja na Lilian Kibona, ambaye ni mke wa Kasekwa.

Katika utetezi wao, washtakiwa hao walidai walikamatwa, kuwekwa kizuizini na kuhojiwa na Jeshi la Polisi kinyume cha sheria.

Huku mshtakiwa wa pili, Kasekwa, akidai maelezo hayo ya onyo yanayobishaniwa mahakamani hapo, hakuyatoa yeye bali alipewa nyaraka zake na kulazimishwa azisaini pasina kujua kilichomo ndani yake.

Kwa upande wa jamhuri, mashahidi walikuwa ni Kamanda wa Jeshi la Polisi Kinondoni, Dar es Salaam, ACP Ramadhan Kingani, aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai mkoani Arusha, wakati washtakiwa hao wanakamatwa.

Wengine ni, aliyekuwa Msaidizi wa Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Arusha, Mahita Omari Mahita na Detective Ricado Msemwa, aliyewapokea watuhumiwa hao walipofikishwa mahabusu katika Kituo Kikuu cha Polisi cha Dar es Salaam, wakitokea Kituo cha Polisi cha Kati Moshi, mkoani Kilimanjaro.

Mashahidi hao wa jamhuri walitoa ushahidi wao mahakamani hapo wakidai kuwa, maelezo hayo ya onyo ni halali, kwa kuwa taratibu za kisheria zilifuatwa wakati mshtakiwa huyo anahojiwa.

Kesi hiyo imeahirishwa ili Jaji Kiongozi Siyani apate muda wa kujadiliana na pande zote za mawakili

Endelea kufuatilia MwanaHALISI TV, MwanaHALISI Online na mitandao yetu ya kijamii kujua kinachoendelea mahakamani hapo

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari za Siasa

Zanzibar mbioni kuanza uchimbaji mafuta na gesi baharini

Spread the loveSERIKALI ya Zanzibar, imekamilisha mchakato wa uchimbaji wa mafuta na...

Habari za Siasa

Wizara ya afya yataja mafanikio 10 miaka mitatu Samia madarakani

Spread the loveWIZARA ya Afya imetaja mafanikio 10 iliyoyapata ndani ya miaka...

Habari za Siasa

Mbozi walilia kuwa manispaa, majimbo 3

Spread the loveHALMASHAURI ya wilaya ya Mbozi mkoani Songwe imeeleza dhamira yake...

Habari za Siasa

Wabunge waitaka TPDC kuongeza kasi ya kuunganisha wateja gesi asilia

Spread the love  KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini...

error: Content is protected !!