Friday , 26 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Uchaguzi Mkuu 2020: Mufti Wa Tanzania awapa neno Waislamu
Habari za Siasa

Uchaguzi Mkuu 2020: Mufti Wa Tanzania awapa neno Waislamu

Aboubakar Zubeir, Mufti wa Tanzania
Spread the love

ABOUBAKAR Zubeir, Mufti Mkuu wa Tanzania, amewaonya watu wanaopanga kufanya vurugu katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Jumatano tarehe 28 Oktoba, 2020. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam…(endelea).

Mufti Zubeir amesema hakuna sababu ya watu kufanya vurugu wala ghasia katika kipindo hicho cha mchakato wa uchaguzi.

Kiongozi huyo wa Waislamu amesema hayo wakati akizungumza katika  Baraza la Eid El Adh’haa  lililofanyika kitaifa kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam, leo Ijumaa tarehe 31 Julai 2020.

Mufti Zubeir amewapasha watu wanaotaka kuwapotosha Waislamu kwamba hawatafanikiwa.

“Hakuna nchi nzuri kama Tanzania, inawezekana huijui ni nzuri sababu labda hujatembea, yawezekana huijui nzuri una mambo yako mengine katika fikra zako nyingine, katika fikra zako sasa unataka kulazimisha watu wakamate fikra zako, muislamu hakamatishwi fikra.”

“Muislamu ameambiwa na mtume ukitaka kufanya jambo kwanza fikiri, muislamu hashikiwi akili, muislamu kazi yake ni kufikiri jambo hilo lina masilahi anahimizwa afanye lenye maslahi,” amesema Mufti Zubeir.

Mufti Zubeir amewahimiza Waislamu kushikamana pamoja na kuienzi amani katika mchakato wa uchaguzi hadi siku ya uchaguzi.

“Lakini pia, nigusie juu ya amani sasa hivi tunaenda kwenye mchakato wa uchaguzi, ni juu yenu Waislamu na mimi nazungumza kama kiongozi wa Waislamu ni juu yenu kujilazimisha kushikama na utulivu na kuyaendea mambo yetu kwa umakini na kuuendea uchaguzi mkuu kwa makini,” amesema Mufti Zubeir.

Naye Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa aliyekuwa mgeni rasmi kwenye Baraza hilo amesema, kila Mtanzania anapaswa kuhakikisha uchaguzi wa mwaka huu unakuwa wa amani na utulivu.

Amesema kuwa kiongozi wa nchi, Rais John Pombe Magufuli amewahakikishia Watanzania kuwa uchaguzi utakuwa wa huru na haki.

“Naamini viongozi wa dini na kila mmoja tunaendelea kuliombea taifa hili ili uchaguzi wa mwaka huu umalizike salama, tujiepushe na lugha za uchochezi, tujiepushe na lugha za bezo, tujiepushe na lugha za kashfa, tuzungumze kile ambacho wananchi hawa utawatendea,” amesema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Prof. Muhongo akomalia matumizi nishati jadidifu kuondoa uhaba wa umeme

Spread the love  MBUNGE wa Musoma Vijijini (CCM), Profesa Sospeter Muhongo, ameendelea...

Habari za Siasa

Kilosa yawa mfano wa kuigwa miradi ya Mwenge nchini

Spread the love  KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa Godfrey Mzava amezitaka...

Habari za SiasaTangulizi

Biteko ataja vipaumbele 7 bajeti nishati 2024/25

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mwekezaji amwaga bil. 39 kujenga viwanda 3 vya uchenjuaji

Spread the loveKampuni ya Mineral Access System Limited (MAST) inayoiwakilishwa kampuni ya...

error: Content is protected !!