May 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Tukio la risasi Dar; IGP Sirro asema askari wawili wafariki dunia

IGP Simon Sirro

Spread the love

 

INSPEKTA Jenerali wa Polisi (IGP), Simon Sirro amesema, askari wawili wamefariki dunia wakati wakimdhibiti mtu mmoja aliyekuwa alifyatua risasi hovyo karibu na Ubalozi wa Ufarasa, Dar es Salaam leo mchana. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

IGP Sirro amesema, mtu huyo naye amefariki dunia kwenye majibizano ya risasi kati yake na askari.

Tukio hilo limetokea mchana wa leo Jumatano, tarehe 25 Agosti 2021, karibu na Ubalozi wa Ufaransa jijini Dar es Salaam na kusababisha taharuki kwa wananchi.

Picha na vipande mbalimbali vya video, vimesambaa mitandaoni vikionyesha mtu huyo akiwa na silaha mbili, moja ikining’inia shingoni na nyingine ameishika mkononi.

James Kolnel, kondakta wa daladala kutoka Makumbusho kwenda Posta, aliyekuwa eneo la tukio amesema “baada ya kuona risasi zinazidi nikaamua kufungua mlango nikawaambia abiria tokeni nje mjitetee wenyewe maana hali halisi mnaiyona.”

error: Content is protected !!