Friday , 29 March 2024
Home Kitengo Michezo Serikali kurudisha tuzo za wasanii, kujenga arena Dar, Dodoma
Michezo

Serikali kurudisha tuzo za wasanii, kujenga arena Dar, Dodoma

Dk. Hassan Abbas, Katibu Mkuu wizara ya Habari
Spread the love

 

KATIBU Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Hassan Abbas amesema serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa sanaa watajikita katika kukuza wa sanaa nchini ikiwamo kurejesha mashindano ya tuzo za wasanii. Anaripoti Matilda Peter, Dar es Salaam … (endelea).

Akiongoza kikao cha majumuisho ya mapendekezo ya kanuni ya leseni ya utangazaji na maonesho kwa umma leo tarehe 25 Agost 2021, jiji Dar es salaam, Dk. Abbas ametaja baadhi ya maeneo muhimu ambayo wataanza kuyaboresha hivi karibuni pia ni mirabaha ya wasanii.

Pia Dk. Abbas amesema kati ya jiji la Dodoma na Dar es salaam kutajengwa ukumbi mkubwa wa matamasha (Arena) na kuboresha miundombinu ya sanaa na kukuza thamani ya muziki nchini.

Aidha, amewataka wasanii wajiandae na tuzo kwa kuwa ni moja kati ya mpango madhubuti wanaotarajia kuurudisha na safari hii wasanii washindwe wenyewe.

“Tumeamua kwa nia njema kabisa na wote tunafahamu kwamba tuzo zilikufa kwa figisu zenu nyinyi wenyewe” amesema Dk. Abbas.

Pia amesema safari hii tuzo zitatolewa na kugawanywa kwenye maeneo yote ya sanaa na kutambua kila mchango wa sanaa zote za Tanzania na pia amewaomba wadau mbalimbali na kuwakaribisha ili kushirikiana na serikali.

Amesisitiza kwamba sanaa inahitaji watu wenye mtazamo chanya kwa ajili ya maendeleo yao na sio mbwembwe au kiki zisizo na faida kwa wasanii.

Amewaomba wasanii kuboresha kazi zao kwani katika tuzo zitakazokuja hakutokuwa na kiki bali kuzingatia ubora wa kazi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Makala & UchambuziMichezo

TFF kuamua hatima ya Amrouche

Spread the loveHATIMA ya Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Adel Amrouche kuendelea...

Habari za SiasaMichezo

Matinyi: Dk. Ndumbaro alifanya utani ukaguzi mechi za Yanga, Simba

Spread the loveMsemaji Mkuu wa Serikali, Mobhare Matinyi amesema kauli iliyotolewa na...

Michezo

Gethsemane Group Kinondoni (GGK) waachia video ya Bwana Wastahili

Spread the loveWAIMBAJI maarufu nchini kutoka Gethsemane Group Kinondoni (GGK)SDA wameachia video...

BiasharaMichezo

Gamondi kocha bora mwezi Februari, NBC yamjaza manoti

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) ambae ni mdhamini Mkuu...

error: Content is protected !!