Thursday , 30 March 2023
Home Kitengo Michezo ‘Top four’ England, kumweka bingwa njia panda
MichezoTangulizi

‘Top four’ England, kumweka bingwa njia panda

Spread the love

WAKATI Ligi Kuu England ikiendelea tena leo ikiendelea leo kwa michezo miwili kupigwa, haki imeonekana si shwari kwa timu kugombania nafasi nne za juu (Top Four) kutokana na kuachana kwa pointi tatu huku hadi sasa bingwa akiwa hatabiliki. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam …  (endelea).

Ligi hiyo ambayo mpaka sasa imecheza michezo 19 kwa baadhi ya timu, itaendelea leo kwa kushudia Manchester United ikiwa ugenini kuwakabili Fulham, huku Manchester City ikiwa nyumbani kuwaalika Astorn Villa.

Msimamo wa Ligi hiyo kwa sasa unaonesha Klabu ya Leceister City ikiwa juu kileleni mara baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-0, mbele ya Chelsea jana ikiwa na pointi 38, huku ikifuatiwa na Manchester United kwenye nafasi ya pili ikiwa na pointi 37 ikiwa nyuma kwa mchezo mmoja.

Nafasi ya tatu kwenye ligi hiyo inashikiliwa na Manchester City mara baada ya kucheza michezo 17, akiwa na pointi 35, huku Liverpool ikiwa kwenye nafasi ya nne kwa pointi 34, mara baada ya kucheza mechi 18.

Kama Manchester United akishinda mchezo wake wa leo dhidi ya Fulham atarejea kileleni kwa pointi 40, akiwa idadi sawa ya michezo na Leicester City.

Kwa upande wa Manchester City wanahitaji kushinda michezo yao miwili ya mkononi ili kuweza kushika usukani wa Ligi kwa kuwa watakuwa wanafikisha jumla ya pointi 41, na kuwa na idadi ya michezo 19 sawa na Manchester United.

Kumbuka Ligi hiyo tayari imeshaingia kwenye duru la pili, huku kukiwa hakuna timu inayopewa kipaumbele kushinda ubingwa huo kwa msimu huu 2021/21, ukilinganisha na msimu uliopita ambao Liverpool walikuwa mabingwa.

Wachambuzi wengi wanaamini Ligi ya msimu huu ni tofauti kwa kiasi cha kupelekea kocha wa kikosi cha Liverpool, Jurgen Klopp kuwaambia mashabiki wa timu hiyo kuwa malengo yake kwa sasa sio kuchukua taji hilo bali kumaliza kwenye nafasi nne za juu.

“Malengo makubwa ni kufuzu kwenye michuano ya klabu bingwa na najua ugumu wake, msimu huu utakuwa na ushindani mkubwa sana kumaliza kwenye nafasi nne za juu,” alisema Klopp.

Liverpool kwa sasa ipo nafasi ya nne kwenye msimamo ikiwa imepishana pointi moja na klabu ya Tottenham ambayo inapointi 33, ikiwa kwenye nafasi ya tano zote zikiwa na michezo sawa.

Na wakati huo huo Liverpool ikiwa na pointi zake 34, imepishana alama mbili na klabu ya Everton yenye pointi 32 ikiwa na michezo 17 na kama ikifanikiwa kushinda mchezo wake wa mkononi itafikisha pointi 35 na kuishusha Liverpool mpaka nafasi ya sita.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

TANROADS wawataka watumishi wazingatie michezo kazini

Spread the love  WAKALA wa barabara Tanzania (TANROADS) imesema michezo inapaswa kuzingatiwa...

Michezo

Yanga: Fedha za Rais Samia zinaleta ari kubwa

Spread the loveUONGOZI wa klabu ya Yanga, umesema fedha zinazotolewa na Rais...

Michezo

Simba Sc. yamvulia kofia Rais Samia, yamuahidi makubwa dhidi ya Horoya

Spread the loveWAKATI timu ya Simba ikiibuka na ushindi wa bao 3-0...

Habari MchanganyikoTangulizi

Rais Samia ampandisha cheo RPC wa Dar

Spread the loveMKUU wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Camillus Wambura, amesema...

error: Content is protected !!