May 20, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mwambusi aachana na Yanga

Juma Mwambusi, kocha msaidizi wa Yanga

Spread the love

KOCHA msaidizi wa timu wa Yanga, Juma Mwambusi ameamua kuachana na klabu hiyo mara baada ya kusumbuliwa na matatizo ya kiafya na kuhitaji kupumzika kwenye nafasi hiyo. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea).

Akithitbitisha taarifa hiyo Mwenyekiti wa klabu ya Yanga, Mshindo Msolla amesema kuwa kocha huyo aliandika barua kwa uongozi kuomba kupumzika wakati timu ikiwa kwenye michuano ya kombe la mapinduzi visiwani Zanzibar mara baada ya kushauliwa na madaktari.

“Aliandika barua wiki mbili zilizopita kuomba apumzike baada ya kushauliwa na madaktari, na ameshauliwa akae nyumbani na hali ikitengemaa atarudi kwenye shughuli zake,” alisema Msolla.

Mwenyekiti huyo aliongezea kuwa mara baada ya kupokea barua hiyo watakaa na Mwalimu mkuu wa timu hiyo, Cedric Kaze kuona kama ataweza kufanya kazi hiyo peke yake mpaka Mwambusi atakapopona au atahitaji msaidizi mwingine.

“Kwa kifupi niseme anapumzika na sisi tutakaa na mwalimu tuone kama anaweza kufanya kazi hiyo mwenyewe au atataka msaidizi kwa hiyo tutamsikiliza,” aliongezea Msolla.

error: Content is protected !!