Friday , 26 April 2024
Home Kitengo Michezo TFF yawatimua wajumbe wanaomtetea Malinzi
Michezo

TFF yawatimua wajumbe wanaomtetea Malinzi

Wallace Karia, Kaimu Rais wa TFF
Spread the love

KAMATI ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imefanya mabadiliko ya Kamati ya Uchaguzi na kuwaengua wajumbe wanne walioonyesha kumtetea Rais wa shirikisho hilo, Jamal Malinzi ambaye kwa sasa yuko rumande kwa tuhuma mbalimbali, anaandika Mwandishi Wetu.

Uamuzi huo umefikiwa baada ya kikao cha Kamati ya Utendaji ya TFF kilichofanyika leo mchana makao makuu ya shirikisho hilo, chini ya Kaimu Rais, Wallace Karia.

Wajumbe walioondolewa ni pamoja na Makamu Mwenyekiti, Wakili Domina Madeli, Juma Lallika, Jeremiah Wambura na Hamim Mahmoud Omar na sasa Mwenyekiti, Wakili Revocatus Kuuli atafanya kazi na Mbunge wa Rufiji, Mohamed Mchengerwa, Wakili Malangwe Ally Mchungahela, Wakili Kiomoni Kibamba ambaye pia ni Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza ma Wakili Thadeus Kalua.

Kabla ya hapo, Mwenyekiti Kuuli alitofautiana na wajumbe wenzake wote wa kamati hiyo ya awali juu ya Malinzi kuruhusiwa kuendelea kuogombea katika uchaguzi wa Agosti 12, mwaka huu mjini Dodoma licha ya kwamba hakutokea kwenye usajili.

Wakili Kuuli alipingana na wenzake waliotaka Malinzi aruhusiwe kuendelea na mchakato japo hakushiriki usaili na kufikia kuvunja kikao, kisha kupeleka taarifa Kamati ya Utendaji ya TFF, ambayo nayo baada ya kikao chake cha leo imefikia uamuzi wa kuiunda upya Kamati ya uchaguzi pamoja na Kamati nyingine.

Sasa Kamati mpya ya Uchaguzi inatarajiwa kuendelea na mchakato, ambao ulisimamishwa kwa muda Julai 2 ukiwa katika hatua ya usaili, bila jina la Malinzi kupita.

Kamati nyingine zilizotajwa na Kaimu Katibu Mkuu wa TFF, Salum Madadi leo ni Kamati Maadili ambayo inaindwa na Mwenyekiti, Amidou Mbwezeleni, Steven Zangira, Mkuu wa Wilaya ya Tarime mkoani Mara, Glorius Luoga, Walter Lungu na Amin Bakhresa.

Kamati ya Rufaa ya Maadili; Wakili Rugemeleza Nshala, Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani, DCP Mohammed Mpinga, Wakili Benjamin Karume, Dk Lisobine Chisongo, ASP Benedict Nyagabona.

Kamati ya Nidhamu; Tarimba Abbas, Peter Hela, Boniface Lyamwike, Dk Billy Aonga na Kassim Dau, Kamati ya Rufaa ya Nidhamu; Wakili Rahim Zubeiry Shaaban, Siza Chenga, Abbas Mtemvu, Amani Mulika na Stella Mwakingwe wakati Kamati ya Rufaa ya Uchaguzi inaundwa na Wakili Abdi Kagomba, Kenneth Mwenda, Rashid Sadallah, Jabir Shekimweri na Mohamed Gombati.

Wakati huohuo: Ujumbe wa Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) hautakuja tena nchini baada ya mazungumzo na Kaimu Rais wa TFF, Wallace Karia kwa njia nya simu.

Karia amesema katika mazungumzo hayo amewaeleza kila kitu kinachoendelea nchini ikiwemo kikao cha leo cha Kamati ya Utendaji na wameridhika na kuitakia kila la heri kamati hiyo.

“FIFA hawatakuja tena, tuliongea nao tukawaeleza kinachoendelea, walitupigia wakitaka kujua kama kulikuwa na muingilio wa serikali katika mchakato, au kama kuna fedha za FIFA zilizotumika vibaya, tukawaambia siyo kweli na kuwaeleza kilichotokea kwa hiyo hawatakuja,” amesema Karia.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

EPL, Ligue 1 na Coppa Italia kinawaka leo

Spread the love  LEO ligi kadhaa zitaendelea nchini barani ulaya ikiwemo ligi...

BiasharaMichezo

NBC yaunga mkono jitihada kutokomeza malaria

Spread the loveKuelekea Maadhimisho ya siku ya malaria Duniani yatakayofanyika kesho Aprili...

Michezo

Arsenal dhidi ya Chelsea ngoma nzito leo EPL

Spread the love  Leo kutakua na mchezo mkali sana pale kwenye ligi...

Habari MchanganyikoMichezo

NBC yanogesha Derby Kariakoo, Aziz Ki aibuka mchezaji bora Machi

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) ambayo ni mdhamini Mkuu...

error: Content is protected !!