Wednesday , 24 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Mbatia alia na ajira mpya za walimu
Habari za Siasa

Mbatia alia na ajira mpya za walimu

James Mbatia, Mbunge wa Jimbo la Vunjo mkoani Kilimanjaro (NCCR-Mageuzi)
Spread the love

JAMES Mbatia, Mbunge wa Jimbo la Vunjo mkoani Kilimanjaro (NCCR-Mageuzi), amesema kuwa tatizo la walimu nchini badoni kubwa sana kwa sasa tofauto na inavyoelezwa na serikali, anaandika Dany Tibason.

Mbatia amesema kuwa inashangaza kuona serikali ikishindwa kupangia walimu vituo vya kazi ilihali wilaya mbalimbali hapa nchini zina uhaba wa walimu, ambapo alieleza kwamba wilaya ya Vunjo pekee ina upungufu wa walimu 207.

Alitoa kauli hiyo bungeni wakati wa kipindi cha maswali na majibu kwa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia ambapo alihoji; “ni lini serikali itaweza kutatua tatizo la uhaba wa walimu ambalo linaonekana kuwa kero kubwa katika maeneo mbalimbali nchini.”

Wakati Mbatia akihoji kuhusu hilo, naye Suzan Lyimo, Mbunge wa Viti Maalum (Chadema), katika swali la nyongeza alitaka kujua ni lini serikali serikali itaweza kufanya mgawanyo sawa wa walimu kwani walimu wengi wapo mijini wakati vijijini kuna upungufu mkubwa wa walimu.

Awali Doto Biteko, Mbunge wa jimbo la Bukombe (CCM), alitaka kujua ni lini serikali itapeleka walimu wa shule za msingi wa kutosha ili kuondoa upungufu uliopo katika wilaya ya Bukombe.

“Wilaya ya Bukombe ina mahitaji ya walimu wa shule za Msingi 1,425 ,kwani waliopo ni 982 na kuna upungufu wa 443.

“Je ni lini serikali itapeleka walimu wa shule za msingi wa kutosha ili kuondoa upungufu uliopo?” alihoji Biteko.

Akijibu maswali hayo ya Biteko, Mbatia na Lyimo, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais –TAMISEMI George Simbachawene alisema kwa sasa TAMISEMI imekuwa ikifanya utaratibu wa kupeleka walimu katika maeneo mbalimbali ambako kuna uhaba wa walimu.

“Tunawapangia walimu vituo vya kazi lakini wengi wanahama katika vituo vyao vya kazi kutokana na kutomudu hali ya miundombinu iliyopo katika sehemu husika ikiwa ni pamoja na halmashauri kushindwa kuwapatia motisha,” amesema Simbachawene.

Selemani Jafo, Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais –TAMISEMI, akitoa majibu ya nyongeza alisema, “Serikali inatambua upungufu wa walimu uliopo nchini ambapo mahitaji ya walimu wa shule za msingi na sekondari kwani waliopo ni walimu 188,481 na upungufu ni walimu 47,151.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Biteko ataja vipaumbele 7 bajeti nishati 2024/25

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mwekezaji amwaga bil. 39 kujenga viwanda 3 vya uchenjuaji

Spread the loveKampuni ya Mineral Access System Limited (MAST) inayoiwakilishwa kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

Mpwa wa Magufuli mbaroni kwa kusambaza picha za utupu

Spread the loveJESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewakamata...

Habari za Siasa

Serikali kuanzisha mradi wa Gridi ya maji ya Taifa

Spread the loveWaziri wa Maji, Jumaa Aweso amesema katika mwaka wa fedha...

error: Content is protected !!