Saturday , 27 April 2024
Home Kitengo Michezo TFF yamjia juu Manara
Michezo

TFF yamjia juu Manara

Clifford Ndimbo, Msemaji wa TFF (kulia) akiwa na Msemaji wa Simba, Haji Manara
Spread the love

SIKU moja tu kufuatia kauli ya Msemaji wa klabu ya Simba, Haji Manara ya kutotaka mashabiki wa timu pinzani kuingia Uwanjani kwenye mchezo dhidi ya Plateau, Shirikisho la Mpira wa Miguu TANZANIA (TFF) imekemea kwa nguvu kauli hiyo kutokana na suala la ubaguzi kutokubalika kwenye mchezo wa mpira wa miguu. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea).

Katika mkutano wake na waandishi wa habari, Manara alisema kuwa katika mchezo huo wa siku ya Jumamosi tarehe 5 Desemba, 2020, hawatoruhusu jezi isiyokuwa rangi nyekundu na nyeupe au mashabiki wasiokuwa wao kuingia uwanjani kwa kuwa mchezo huo ni wao.

Kauli hiyo ya msemaji huyo imekuja mara baada ya mashabiki wa Yanga ambao ni wapinzani wao kuonekana kutaka kwenda kuwashabikia wageni hao na hata baadhi yao kuonekana kununua na kuvaa jezi ya timu hiyo ambayo ni mabingwa wa Ligi Kuu nchini Nigeria.

Taarifa kutoka ndani ya TFF imeeleza kuwa kwa mujibu wa katiba ya Shirikisho la Mpira Dunia (Fifa) na TFF vitendo vyovyote vya ubaguzi havikubariki kwenye mpira wa miguu.

Aidha taarifa hiyo imeendelea kueleza kuwa shabiki yoyote anaruhusiwa kuingia kwenye mechi ya mpira wa miguu ikiwa tu hatovunja sheria na taratibu.

Simba itashuka uwanjani siku hiyo kucheza mchezo wa klabu bingwa barani Afrika kwenye hatua ya awali dhidi ya Plateau kwenye mchezo wa mzunguko wa pili mara baada ya kuibuka na ushindi wa bao 1-0, kwenye mchezo wa kwanza uliochezwa mjini Jos, Nigeria.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

EPL, Ligue 1 na Coppa Italia kinawaka leo

Spread the love  LEO ligi kadhaa zitaendelea nchini barani ulaya ikiwemo ligi...

BiasharaMichezo

NBC yaunga mkono jitihada kutokomeza malaria

Spread the loveKuelekea Maadhimisho ya siku ya malaria Duniani yatakayofanyika kesho Aprili...

Michezo

Arsenal dhidi ya Chelsea ngoma nzito leo EPL

Spread the love  Leo kutakua na mchezo mkali sana pale kwenye ligi...

Habari MchanganyikoMichezo

NBC yanogesha Derby Kariakoo, Aziz Ki aibuka mchezaji bora Machi

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) ambayo ni mdhamini Mkuu...

error: Content is protected !!