April 21, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Sabaya aagiza mabaraza ya ardhi kuvunjwa

Lengai Ole Sabaya, Mkuu wa Wilaya ya Hai

Spread the love

MKUU wa Wilaya ya Hai Mkoa wa Kilimanjaro, Lengai Ole Sabaya, ameagiza kuvunjwa kwa mabaraza ya ardhi kata za Kia na Mnadani wilayani humo kutokana na migogoro ya ardhi inayosababishwa na mabaraza hayo. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Sabaya ametoa maagizo hayo jana Jumatano tarehe 2 Desemba 2020 wakati akizungumza na madiwani 24 wa Halmashauri ya wilaya ya Hai ,muda mchache baada ya hafla ya kuwaapisha madiwani hao.

“Tatizo kubwa ambalo lipo hapa Hai ni migogoro ya ardhi, nimwagize katibu tawala wangu avunje mabara yote ya kata za Kia na Mnadani ili wote tuwe sawa.”

“Haiwezekani mteke nyara mali za wajane na mayatima kwa manufaa yenu wenyewe, bora wote tuwe maskini bora kama ni mali ya haki kila mtu ajue ni mali ya haki,” alisema Sabaya

Hata hivyo, alimtaka mbunge wa Jimbo hilo pamoja na Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo kwenda kutatua migogoro ya wananchi na kutekeleza ahadi za wananchi na zile ambazo Rais John Magufuli aliwaahidi wakazi wa wilaya hiyo.

“Viongozi wote wa Wilaya hii ambao mmepewa dhamana na Serikali ya kuwatumikia wananchi wa Jimbo hili, nendeni mkatatue changamoto za wananchi wa Hai, tekelezeni ahadi ambazo alizitoa kwa wananchi,” alisema Sabaya

error: Content is protected !!