Saturday , 4 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Tanzania yapongezwa kurejesha amani DRC, ICGLR
Habari Mchanganyiko

Tanzania yapongezwa kurejesha amani DRC, ICGLR

Spread the love

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imepongezwa kwa kuendelea kuwa mstari wa mbele kurejesha amani katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na Ukanda wa Maziwa Makuu. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).

Pongezi hizo zimetolewa Mjumbe Maalum wa Katibu Mkuu Umoja wa Mataifa katika Ukanda wa Maziwa Makuu, Balozi Huang Xia alipokutana na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, January Makamba – Jijini Dar es Salaam.

“Umoja wa Mataifa tunaipongeza Tanzania kwa kulinda misingi ya amani na kuwa mstari wa mbele katika kurejesha amani na usalama katika Ukanda wa Maziwa Makuu,” alisema Balozi Huang.

Huang ameongeza kuwa ni wakati muafaka kwa viongozi wa Ukanda wa Maziwa Makuu kusaidia kuhakikisha kuwa amani inapatikana Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ili kuliwezesha taifa hilo kusonga mbele kiuchumi na kisiasa.

Kwa upande wake Waziri Makamba ameupongeza Umoja wa Mataifa kwa kuendelea kudumisha amani katika ukanda wa Maziwa Makuu kwani ndiyo njia itakayosaidia kuwalinda raia na kukuza uchumi katika ukanda huo.

“Tanzania chini ya uongozi imara wa Rais, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, inaamini amani ndio msingi pekee wa maendeleo kwa mtu mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla,” alisema Waziri Makamba.

Pamoja na mambo mengine, Waziri Makamba amemhakikishia Balozi Huang kuwa Tanzania itaendelea kushirikiana na Umoja wa Mataifa na Jumuiya za Kimataifa na za Kikanda kurejesha amani na usalama katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na Ukanda wa Maziwa Makuu.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

RPC Dodoma akabidhiwa bunduki mbili za wahalifu

Spread the love  Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa ya Kulevya...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NBC yazindua huduma maalum kwa wastaafu

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) imezindua huduma maalum kwa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB yazindua akaunti ya Kikundi

Spread the loveBenki ya NMB imezindua akaunti ya kikundi yenye  maboresho makubwa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Wafanyakazi waidai STAMICO mishahara ya bilioni 1

Spread the loveWALIOKUWA wafanyakazi wa mgodi wa Shirika la Madini la Taifa...

error: Content is protected !!